KABLA HUJACHUKUA MKOPO WA NYUMBA JUA UNATAKA KUJENGA NINI

Kati ya mikopo mikubwa ambayo watu na hasa waajiriwa huchukua mapema ni pamoja na mikopo ya nyumba, mikopo hii huchukuliwa mara nyingi zaidi kwa ajili ya kujenga nyumba za kuishi kuliko nyumba za biashara na nyinginezo. Hata hivyo bado sio wazo la busara kwenda kuchukua mkopo wa nyumba kabla hujajiandaa vizuri kwa kufahamu ni nini hasa unahitaji na kwa viwango gani.

Unaweza kukutana na mtaalamu wa ujenzi kabla ya kuchukua mkopo wa nyumba ili mjadili sana kwa kirefu kuhusu mradi husika na kupata kujua kwa usahihi ni kiasi gani cha fedha utakachohitaji kutokana na namna ulivyochagua vitu vitakavyojumuika kwenye jengo.

Hata kwa majengo ya biashara pale unapokutana na mtaalamu na kujadili kwa kirefu kujua kile hasa uanchotaka katika jengo lako utapata mwanga mkubwa sana pale unapoenda kwenye taasisi ya kifedha kuomba mkopo na kujieleza kwa kujiamini kabisa juu ya kiasi cha fedha unachohitaji na utafanyia nini na nini hasa. Karibu sana tushauriane kwa usahihi kabla hujachukua mkopo wa nyumba kutoka kwenye taasisi za kifedha au kwingineko.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *