FIKIRI KWA USAHIHI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI.

Kawaida gharama za ujenzi wa nyumba mpaka inakamilika huwa ni kubwa, kwa ujumla kujenga nyumba sio kitu unaweza kukilinganisha na vitu kama kununua gari au kununua kiwanja kwani gharama za ujenzi ni kubwa sana mpaka nyumba kukamilika. Ukubwa wa gharama hizi umekuwa ukiwafanya watu kufikiria sana namna ya kuzipunguza kwa njia mbalimbali na hapa ndipo watu hukosea juu ya namna sahihi za kupunguza gharama hizi japo watu wengi hawajui hata uhalisia wa gharama za zenyewe zilivyo.

UNAPASWA KUFAHAMA GHARAMA ZA UJENZI KATIKA UHALISIA KABLA YA KUFIKRIA KUZIPUNGUZA

Sehemu ambayo watu hukimbilia sana wanapofikria kupunguza gharama za ujenzi ni kwenye kupunguza gharama za tofali kwa kufikiria kwamba ni moja ya sehemu inayopelekea gharama kubwa sana. Wengi hufikiria labda wakitumia tofali za kuchoma watapunguza sana gharama za ujenzi au labda wakitengeneza tofali wenyewe labda watapunguza gharama za ujenzi, lakini hili ni kosa la kutofikiria katika picha kubwa juu ya gharama za mradi mzima.

GHARAMA ZA TOFALI NI SEHEMU NDOGO SANA YA GHARAMA ZA UJENZI WA JENGO LOTE MPAKA KUKAMILIKA

Tofali kama tofali ni sehemu ndogo sana ya gharama za ujenzi tofauti na wengi wanavyofikiri na unapomaliza kujenga tofali katika nyumba yako bado uko mwanzoni kabisa katika kukamilisha ujenzi huo. Kwa mfano nyumba ambayo ujenzi wake mpaka kukamilika na kuhamiwa inaweza kujengwa kwa jumla ya Tshs milioni 100, gharama ya tofali za nyumba nzima haiwezi kuzidi Tshs milioni 5 yaani ni chini ya asilimia 5% ya ujenzi wa nyumba nzima. Hapa unaweza kuona kwa mfano hata gharama ya kuezeka peke yake inaweza kuwa kubwa hata kuzidi gharama ya tofali za nyumba nzima. Hivyo inapofikiria kuhusu namna ya kupunguza gharama za ujenzi ni makosa kufikiria kwamba ukijitahidi kupata tofali kwa bei nafuu utapunguza gharama za kujenga na badala yake unapaswa kufikiria kwamba katika kila hatua ya ujenzi unawezaje kupunguza hapo gharama kiasi ili mwisho wa siku ukichanganya vyote ukute umepunguza sehemu kubwa kidogo ya gharama hizo kwa ujumla.

GHARAMA YA KUWEKA TILES PEKE YAKE INAWEZA KUFIKA ZAIDI YA MARA MBILI YA GHARAMA YA TOFALI

Jambo la muhimu ni kujitahidi usije kulazimisha kupunguza sana gharama na kusababisha ujenzi mbovu, kupunguza gharama kusicheze mbali na ubora wa nyumba yenyewe.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *