FAIDA ZA TOFALI ZA KUCHOMA
Ni nyepesi
Katika ujenzi uzito wa tofali unasababisha kazi inaenda taratibu na fundi kuchoka haraka, tofali za kuchoma ni nyepesi hivyo mtu anaweza kuzijenga kwa haraka na kwa wingi zaidi bila kuchoka kiurahisi n ahata kazi ikafanyika kwa usahihi kwa sababu ya wepesi wa tofali zenyewe. Hata hivyo kwa kawaida tofali za kuchoma ni ndogo hivyo zinakwenda nyingi sana na kufanya kazi kuwa kubwa.
Mara nyingi ni imara
Japo uimara wa tofali unategemeana na mambo mengi kuhusika katika mchakato mzima wa kuzitengeneza lakini mara nyingi uwezekano wa tofali za kuchoma kuwa imara zaidi kuliko tofali za mchanga na saruji ni mkubwa zaidi kwa sababu tofali za kuchoma hazina gharama kubwa sana na kuzifanya kuwa imara hakuambatani na gharama kubwa kama kuzifanya tofali za bloku kuwa imara. Hivyo mara nyingi bila kutumia gharama kubwa tofali za kuchoma huwa imara zaidi na kudumu miaka mingi sana.
Gharama za ukarabati
Gharama za ukarabati wa tofali za kuchoma uko chini sana ukilinganisha na tofali za saruji na mchanga kwa sababu huwa hazihitaji ukarabati wa mara kwa mara na kama zimetumika kama urembo wa nje basi nyumba haitahitaji kutumia pesa nyingi katika kuboresha muonekano wake.
Ubomoaji wake
Ikifikia hatua kwamba jengo litahitaji kubomolewa, ubomoaji wa tofali za kuchoma huwa ni rahisi na mara nyingi hasa kama tofali zilikuwa imara husaidia kupata kuokoa tofali nyingi zaidi ambazo huweza kutumika tena kutokana na saizi yake ndogo huepusha kuvunjika kwa urahisi.
Kwenye kushambuliwa na moto
Pale inapotokea ajali ya moto na jengo kuungua tofali za kuchoma tofali za kuchoma mara nyingi hubaki imara na kutoathirika sana na moto kwani hazishiki moto. Linapoungua jengo lililojengwa na tofali za kuchoma utakuta kila kitu kimeungua lakini tofali zimebaki zikiwa zimesimama na ziko salama. Hili husaidia tofali hizi kuweza kutumika tena au jengo lililoungua kufanya ukarabati bila kuanzia chini.
Mahusiano yake na mazingira
Mchakato mzima wa utengenezaji wa tofali za kuchoma hauhusishi matumizi makubwa na nishati yanayopelekea uchafuzi wa mazingira hivyo tofali za kuchoma zinaepusha kwa kiasi kikubwa swala zima la uchafuzi wa mazingira.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!