CHANGAMOTO ZA MATOFALI YA KUCHOMA

Kutumia muda mwingi kwenye kujenga

Matofali ya kuchoma ni madogo madogo kwa saizi ambapo yanaingia mengi zaidi karibu hata mara mbili ya matofali ya bloku hivyo inachukua muda mrefu sana kukamilisha kazi kwa sababu matofali ya kujenga ni mengi.

WINGI WA TOFALI ZINAZOJENGWA UNASABABISHA KUTUMIA MUDA MWINGI ZAIDI KUKAMILIKA

Usahihi wa kazi

Matofali ya kuchoma yanapaswa kutengenezwa kwa umakini mkubwa yawe katika usahihi wa kiwango cha juu na yawe na ukubwa unaolingana kwa usawa ili kuta ziwe zimenyooka vizuri na kama itapigwa ripu(plasta) isilete gharama kubwa sana katika kulazimisha kunyoosha ukuta uliopinda kwa sababu ya viwango duni vya tofali.

INAHUSISHA GHARAMA KUBWA KWENYE KUPIGA RIPU(PLASTA) HASA ZINAPOKUWA HAZIKO KATIKA UKUBWA UNAOLINGANA

Kusafisha ukuta wa matofali ya kuchoma

Ikiwa ukuta wa matofali ya kuchoma haukufanyiwa “finishing” na badala yake tofali zenyewe zimebakia kama sehemu ya urembo wa nyumba basi huhitaji kufanyiwa usafi mara kwa mara kuiweka nyumba katika hali ya unadhifu. Kazi ya kusafisha tofali hizi huwa ni ngumu na inahitaji muda mwingi sana.

NI KAZI KUBWA NA NGUMU KUSAFISHA UKUTA WA TOFALI ZA KUCHOMA AMBAO HAUJAPIGWA RIPU(PLASTA)

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

1 reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *