CHANGAMOTO ZA MATOFALI YA KUCHOMA
Kutumia muda mwingi kwenye kujenga
Matofali ya kuchoma ni madogo madogo kwa saizi ambapo yanaingia mengi zaidi karibu hata mara mbili ya matofali ya bloku hivyo inachukua muda mrefu sana kukamilisha kazi kwa sababu matofali ya kujenga ni mengi.
Usahihi wa kazi
Matofali ya kuchoma yanapaswa kutengenezwa kwa umakini mkubwa yawe katika usahihi wa kiwango cha juu na yawe na ukubwa unaolingana kwa usawa ili kuta ziwe zimenyooka vizuri na kama itapigwa ripu(plasta) isilete gharama kubwa sana katika kulazimisha kunyoosha ukuta uliopinda kwa sababu ya viwango duni vya tofali.
Kusafisha ukuta wa matofali ya kuchoma
Ikiwa ukuta wa matofali ya kuchoma haukufanyiwa “finishing” na badala yake tofali zenyewe zimebakia kama sehemu ya urembo wa nyumba basi huhitaji kufanyiwa usafi mara kwa mara kuiweka nyumba katika hali ya unadhifu. Kazi ya kusafisha tofali hizi huwa ni ngumu na inahitaji muda mwingi sana.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Tryphone nditegeyeko Rulimbiye