UMUHIMU WA MAWASILIANO SAHIHI KATIKA UJENZI

Katika kila hatua ya mradi wa ujenzi kuanzia hatua ya kwanza ya kutengeneza “concept” na kuandaa michoro ya ramani kuna maamuzi muhimu ambayo huhitajika kufanyika kutoka kila upande unahusika na mradi wa ujenzi. Maamuzi haya ni muhimu na huhitajika kufanyika ila kazi iweze kuendelea katika uelekeo sahihi ambao umekubalika na pande zote.

KILA HATUA YA MRADI WA UJENZI HUHITAJI KUFANYIKA MAAMUZI MUHIMU

Kuwepo kwa mawasiliano yenye ubora kati ya pande zote zinazohusika na ujenzi ndio huwezesha na kurahisisha maamuzi haya katika hatua husika ya ujenzi. Kuchelewa kufanyika kwa maamuzi haya muhimu kutokana na kukosekana kwa mawasiliano sahihi na kwa muda sahihi hupelekea kuchelewesha kazi ambako huambatana na hasara ya muda na fedha au kazi kuelekea uelekeo usio sahihi kutokana na maamuzi yaliyofanywa na watu wasio sahihi na hivyo kupelekea kuharibu kazi kitu ambacho aidha kitasababisha matokeo yasiyotarajiwa ya mradi husika au hasara ya kubomoa na kurudia kazi husika.

Hivyo tangu mwanzoni mwa mradi kunatakiwa kuwe na maandalizi sahihi ya kimawasiliano katika hatua zote za mradi ili kuepuka kazi kuharibika au hasara ya muda na fedha itakayosababishwa na kubomoa na kurudia upya hatua husika ya mradi.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *