FAIDA ZA KUTUMIA FALSAFA YA UJENZI YA “LEAN CONSTRUCTION”.
Falsafa ya ujenzi ya “lean construction” inaleta mapinduzi katika kila hatua ya mchakato mzima wa ujenzi ambapo inahitaji kila timu inayofanya kazi kwenye mradi wa ujenzi kuja pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuweka ubunifu na ufanisi wa hali juu katika mradi husika. Matokeo yatakayotokana ya falsafa ya ujenzi ya “lean construction” yatakayotokana na namna falsafa hii inatekelezwa na manufaa yake yanajumuisha:
-Mradi wa ujenzi kumalizika ndani ya muda uliopangwa: Kwa kuondoa uzembe na kufunika udhaifu kwa kufanya kazi kama timu kinapelekea mradi kumalizika ndani ya muda uliopangwa hata kwa idadi ndogo ya wafanyakazi. Hili ni la muhimu kutokana na ukweli kwamba kampuni nyingi hushindwa kumaliza mradi ndani ya muda uliopangwa kwa sababu ya kukosa watu wenye uwezo mkubwa.
-Kazi kufanyika kwa ubora wa hali ya juu: Kuweka viwango vya juu vya ubora, maboresho endelevu, na kuweka msisitizo kwenye mawasiliano inapelekea timu zinahusika na mradi kupunguza sana makosa ya kiutendaji na kuleta matokeo bora sana.
-Inaongeza sana kuridhika kwa wafanyakazi: Wafanyakazi wanapokuwa na udhibiti mkubwa wa mchakato mzima wa ujenzi, na kuepuka kupoteza muda kwenye kazi ndogo ndogo zisizo na umuhimu, wanakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufurahia kazi zao na hivyo kuweka nguvu na umakini wao wote kwenye kazi husika na kupelekea matokeo bora sana.
-Kudhibiti hatari mapema: Kampuni zinazotumia falsafa ya ujenzi ya “lean construction” huanza kuzipangilia changamoto mapema hata kabla hazijatokea. Suala la kupangilia namna ya kukabiliana na changamoto hata kabla haijatokea husaidia kupunguza kupaniki pale changamoto husika inapotokea na tayari njia mbadala inakuwa imeshaandaliwa.
Kwenye makala ijayo tutajifunza namna ya kuingiza falsafa hii ya ujenzi ya “lean construction” kwenye utekelezaji.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!