KUJENGA MAKAZI NA NYUMBA NI ASILI YA BINADAMU TANGU KALE.

Kumiliki makazi na nyumba imekuwa ni sehemu muhimu sana ya utamaduni wa binadamu tangu kale na kale. Kujenga nyumba na makazi vimeanza tangu kabla ya historia inayojukana kuanza kuandikwa lakini ubunifu na mapinduzi zaidi ya ujenzi yalifanyika katika nyakati zinazojulikana zaidi kihistoria kama “Neolithic period” ambacho ni kipindi cha kati ya miaka 10,000 iliyopita na miaka 2,000 kabla ya kristo.

NYUMBA ZA MWANZO ZAIDI HUKO SUMERIA/BABELI YA KALE ILIYOJENGWA MIAKA ZAIDI 4,000 ILIYOPITA

Wakati huu wa “Neolithic” ndio wakati ambapo ubunifu mwingi na mapambo vilishamiri zaidi katika nyumba na mapambo na viliendelea kuboreshwa kuendana na mila, desturi na tamaduni za jamii hizo za zamani.

MTAA WA NYUMBA HUKO BABELI YA KALE ZAIDI YA MIAKA 4,000 ILIYOPITA

Mapinduzi zaidi ya kujenga yameendelea kuja zaidi na zaidi na suala la kujenga nyumba limekuwa ni sehemu muhimu sana ya utamaduni wa binadamu mpaka sasa. Hata hivyo kutokana na kubadilika kwa tamaduni na mahitaji ya binadamu nyumba na makazi vimeendelea kupitia mapinduzi mengi mbalimbali mpaka nyakati tunazoishi sasa nab ado mapinduzi zaidi yanaendelea kuja kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia katika ujenzi na vifaa vya ujenzi.

MJI KATIKA BABELI YA KALE MIAKA ZAIDI YA 4,000 ILIYOPITA

Mapinduzi haya yameleta mabadiliko makubwa ya kimuonekano ya miji na makazi kitu ambacho kimeendelea kuhamasisha ubunifu zaidi na kukua na kuanguka kwa tamaduni mbalimbali.

MAJENGO MBALIMBALI KATIKA RUMI YA KALE ZAIDI YA MIAKA 2,000 ILIYOPITA

Hivyo ni jambo la kawaida na ni sehemu ya asili ya binadamu mtu kujenga na kumiliki nyumba.

MJI WA KISASA KUALA LUMPUR, MALAYSIA MWAKA 2021

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +25571745270.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *