UZURI WA JENGO NI MUUNGANIKO WA VIPENGELE VYOTE VINAVYOUNDA MUONEKANO WAKE.

Mpangilio na muonekano wa vipengele na muundo unaokamilisha muonekano wa jengo ndio umekuwa unaamua uzuri na mvuto wa muonekano wa jengo husika(building aesthetics). Mpangilio sahihi, vipengele sahihi na vinavyoendana pamoja na muundo sahihi ndio huleta ule mvuto unaovutia sana.

MPANGILIO SAHIHI WA VIPENGELE VYA JENGO NDIO UZURI WENYEWE

Watu kukosa uelewa wa jambo hili imekuwa ni chanzo cha kufanyika kwa majengi yasiyokuwa na mvuto au unakuta ramani na picha zilizoandaliwa zinavutaia vizuri lakini wakati wa utekelezaji ujenzi kwa sababu mbalimbali baadhi ya vipengele vinabadilishwa au kuondolewa na kuharibu muonekano mzima wa jengo.

KUONDOA AU KUBADILISHA VIPENGELE VYA JENGO KUNAHARIBU MUONEKANO WAKE

Hivyo wakati wowote ukifikiria kuandaa ramani ya jengo ni muhimu kuwa na uelewa kwamba namna vipengele vinavyopangiliwa kwa ukubwa na kwa usahihi ndivyo vitakavyoamua uzuri wa muonekano wa jengo na katika kujenga utekelezaji panalazimika kuwepo mtaalamu hasa aliyefanya kazi husika kuhakikisha kila kipengele kinachoamua uzuri ule kinakuwepo katika usahihi wake bila kukiondoa au kukibadili kwa namna yoyote kwani hilo litafifisha uzuri wa jengi husika.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *