NADHARIA YA USANIFU MAJENGO NA UJENZI.

Nadharia ya usanifu majengo na ujenzi ni ile elimu ya nadharia kuhusu majengo na ujenzi, vile namna majengo kwa ujumla yanaweza kuelezewa kwa namna mbalimbali kama vile muundo wake, aina na staili yake, utamaduni husika uliopelekea jengo hilo kuwa na muonekano, muundo, vipimo na urembo unawakilishwa na jengo husika.

NADHARIA YA JENGO INALETA TAFSIRI NA UELEWA MPANA ZAIDI WA JENGO

Nadharia ya usanifu majengo na ujenzi inatusaidia kufahamu mengi kuhusu majengo, historia zake, umuhimu wake katika historia na tamaduni husika na umuhimu wake na maana yake kwa sasa, nadharia ya usanifu majengo inasaidia hata kutoa taarifa zaidi kwa wanahistoria na wanaakiolojia ambao wanahitaji kupata taarifa zaidi juu ya matukio na tafsiri mbalimbali kihistoria zinazoweza kuongeza wigo wa uelewa juu ya kilichokuwa kinaendelea nyakati husika.

ELIMU YA NADHARIA JUU YA JENGO INAONGEZA SANA UELEWA WA HISTORIA, NYAKATI NA LENGO LA JENGO HUSIKA.

Kufahamu nadharia za ujenzi kwa viwango vya mtu binafsi na hata taasisi kunatoa fursa ya mtu au taasisi kuwa kwenye nafasi ya kufanya maamuzi sahihi zaidi katika kuchagua aina au mtindo wa jengo au majengo wanayoyahitaji kulingana na tafsiri husika na tamaduni za aina mbalimbali za vipengele vinavyounda muonekano wa jengo. Kwa mfano kwa mtu binafsi anapata nafasi ya kufahamu kwa nini nyumba yake iwe na muundo, mtindo au mpangilio fulani wa vipengele katika jengo, lakini ambavyo pia vinaleta uzuri katika jengo badala ya kuvutia na uzuri. Kama ni taasisi kama vile ya kidini au hata kiserikali au za kiraia inapata nafasi ya kuamua kwa nini wachague aina fulani kadiri ya tafsiri yake inavyoendana na kile kinacholengwa.

NADHARIA YA JENGO INATAFSIRI MAANA NA UMUHIMU WA VIPENGELE VINAVYOUNDA MUONEKANO WA JENGO KWA LENGO HUSIKA.

Hivyo kufahamu nadharia ya usanifu majengo na ujenzi kunasaidia kuona jinsi jengo husika linaongea na kuweza kuona lugha yake na kusikia sauti yake.

NADHARIA YA USANIFU MAJENGO NA UJENZI INAONYESHA JINSI JENGO LINAONGEA, KUELEWA LUGHA YAKE NA HATA KUSIKIA SAUTI YAKE.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *