HAIHITAJI GHARAMA KUBWA KUFANIKISHA UJENZI BORA WENYE VIWANGO.

Watu wengi huogopa sana wataalamu hasa linapokuja suala la kusimamia kazi katika hatua ya ujenzi ambapo kitu kikubwa wanachokwepa au kuogopa ni gharama za kumlipa mtaalamu huyo, lakini hata hivyo kuna kitu kimoja muhimu sana wanakosea kwamba kazi ili iwe nzuri inahitaji usimamizi sahihi.

USIMAMIZI WA KITAALAMU UNA GHARAMA LAKINI UNAKUPATIA THAMANI KUBWA KULIKO GHARAMA YENYEWE

Kuhusu bei kwanza unachopaswa kujua ni kwamba bei unayolipa inalingana na thamani unayopata lakini mara nyingi unapata thamani kubwa sana zaidi ya ile bei unayolipa. Lakini hata hivyo kama unaogopa beo basi angalau unaweza kumshawishi mtaalamu kukagua tu kazi katia hatua muhimu chache kuanzia mpaka ujenzi unakamilika, yaani mtaalamu anakuja kama mara 3 au 4 peke yake kwenye kila hatua hivyo unamlipa mara hizo chache ambapo bado atakuwa ameongeza thamani kubwa sana tofauti na kukosekana kabisa na gharama utakazomlipa ni kidogo sana ukilinganisha na gharama za huduma nyingine yoyote ya ujenzi huo.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *