JENGO LINATAKIWA KUWA NA UWIANO NA MTIRIRIKO SAHIHI

Tunapozungumzia kuhusu jengo tunazungumzia kuhusu mpangilio wa vipengele vyote vinavyounda jengo husika bila kujali kama vimepangiliwa kwa usahihi au kimakosa. Tunapozungumzia uzuri wa jengo tunazungumzia mpangilio sahihi wa vipangele vyote vya kisanifu vinavyounda jengo husika.

VIPENGELE NDIO VINAAMUA MUONEKANO WA JENGO

Sasa jengo lolote lililofanyika katika viwango na lenye ubora, mvuto na lenye muonekano unaoleta maana ni lazima liwe katika uwiano na mtiririko sahihi. Uwiano(balance) ni ile hali ya jengo kuwa na upacha, utatu na kuendelea katika mpangilio wa kipengele chochote kinachokuwepo juu, chini, kulia au kushoto wa kila kipengele. Mtiririko ni uwepo wa kipengele au vipengele ambavyo vimepangilia katika viwango vya juu sana vya usanifu ambavyo vinaleta ladha nzuri ya kuvutia sambamba na maana fulani ambayo inaongeza umuhimu fulani na kuleta lugha ya jengo inayoongea.

VIPENGELE VILIVYOPANGILIWA KWA USAHIHI NDIO VINALETA UZURI WA JENGO

Hivyo jengo lenye uwiano na mtiririko sahihi ni jengo lililokamilika kwenye kila idara na linalojumuisha vipengele ambavyo vyote vina maana na umuhimu fulani na kuondoa kabisa vipengele visivyo na maana wala umuhimu wowote katika jengo pamoja na muonekano wa jengo.

VIPENGELE VISIVYO NA MAANA WALA UMUHIMU VINATAKIWA KUONDOLOEWA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *