KIPENGELE CHOCHOTE KISICHO NA UMUHIMU KWENYE MUONEKANO WA JENGO KIONDOLEWE.

Siku chache zilizopita nilijadili kwenye makala kwamba mifumo yote inayosambaza huduma ndani ya jengo haipaswi kuonekana kwa nje na badala yake inapaswa kufichwa ndani ya mifereji wima na mifereji mlalo katikati ya nguzo au kwenye kona za jengo ambapo zitabaki kuonekana kama urembo peke yake ili kuboresha muonekano wa jengo ulio rahisi, wenye kuvutia na wenye maana inayokusudiwa.

JENGO LIKIKOSA MPANGILIO SAHIHI WA VIPENGELE VYAKE LINAPOTEZA UBORA WAKE

Lakini changamoto hii ya kuharibika kwa muonekano wa jengo haisababishwi na mifumo inayosambaza huduma ndani ya jengo peke yake licha ya kwamba changamoto ya mifumo inayosambaza huduma mbalimbali ndani ya jengo ndio iliyozoeleka zaidi, viko vipengele vingine mbalimbali ambavyo huwekwa na kuharibu sana muonekano wa jengo. Vitu kama mbao za matangazo, bendera, masahani makubwa ya mawasiliano, pamoja na vipengele vingine mbalimbali huchangia kuharibu au kudhoofisha muonekano wa jengo husika.

KILA KIPENGELE KISICHO NA UMUHIMU KWA NJE KINATAKIWA KUTAFUTIWA MBADALA WAKE

Mpangilio sahihi na unaoleta maana inayokusudiwa ya muonekano wa jengo hautakiwi kuathiriwa na kitu chochote kinachowekwa bila kuwa na maana au umuhimu unaohitajika. Ziko njia nyingi mbadala za kuepuka kuweka vipengele visivyohitajika wala kuwa na umuhimu kwenye muonekano wa jengo ambazo zinaweza kufuatwa ili kuepuka kuliharibu jengo. Ikiwa mtaalamu wa kutengeneza michoro ya ramani ameshindwa kutafuta njia mbadala wa kuliepusha jengo na vipengele visivyo na umuhimu kwa kutokuweka ubunifu wa kutosha katika kazi husika yafaa kazi hiyo ijadiliwe zaidi kwa ushirikiano na mteja pamoja na wataalamu wengine ili changamoto hiyo itatuliwe kuharibu muonekano wa jengo ambalo pesa nyingi sana zinaenda kutumika kulijenga.

MJADALA WA KUTAFUTA MBADALA WA BAADHI YA VIPENGELE ILI KUBORESHA MUONEKANO UNATAKIWA KUSHIRIKISHA WAHUSIKA WENGI ZAIDI KULIKO KUMWACHIA MTAALAMU WA MICHORO YA RAMANI PEKE YAKE IKIWA NI CHANGAMOTO ANAYOSHINDWA KUITATUA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *