MNG’AO KWENYE PICHA UNAOPELEKEA MNG’AO KWENYE UHALISIA NDIO MVUTO WA JENGO

Watu huvutiwa sana na muonekano mzuri unaovutia kwenye jengo bila kujua kile hasa kinachochangia wao kuvutiwa kiasi hicho na uzuri unaoonekana. Uzuri wa jengo unahusisha vitu vikubwa viwili, kimoja ni mpangilio sahihi wa vipengele vya jengo unaofuta mtiririko na uwiano unaoleta maana fulani ya kibunifu au kifalsafa na cha pili ni mng’ao wa kiwango cha juu unajumuisha mpangilio wa rangi unaoletwa na kazi kubwa iliyofanyika ya kufikia mng’ao huo kupitia umakini mkubwa uliowekezwa.

MUONEKANO WA KUNG’AA NI SEHEMU MUHIMU YA MVUTO WA JENGO

Sasa ukiondoa mpangilio sahihi wa vipangele vinavyounda muonekano wa jengo, uzuri wa jengo iwe ni kwenye picha au jengo linalojengwa unachangiwa sana na mng’ao mkubwa na mpangilio wa rangi sahihi unaoletwa na kazi kubwa ya kibunifu inayohusisha umakini wa hali ya juu inayofanywa kwa muda mrefu na kwa utulivu katika kufikia viwango vya juu.

JENGO KUNG’AA KUNAHUSISHA KAZI KUBWA NA UBUNIFU WA HALI YA JUU

Hivyo unapolenga kupata kitu kizuri na chenye kuvutia sana basi unapaswa kufahamu ni kazi inayohusisha ubunifu na utulivu wa hali ya juu iwe ni katika picha au katika uhalisia ili kufikia mng’ao mkubwa wenye kuvutia kama matokeo ya mwisho ya kazi husika.

IWE NI KATIKA PICHA AU KWENYE UHALISIA JENGO LINALONG’AA LINAHUSISHA KAZI KUBWA SANA YA KIBUNIFU

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *