KAZI NZURI INAHITAJI UMAKINI, MUDA NA UTULIVU MKUBWA.

Watu wengi kwa sababu ya kutokutafakari kwa usahihi hawajui kwa nini kazi nzuri huwa na gharama zaidi kuliko kazi ya kawaida, au kusema kwa nini kazi tofauti hutofautiana ubora na bei. Hii inapelekea watu kushindwa kuipa kazi husika uzito unaostahili na utofauti wake.

KAZI YENYE UBORA NI MATOKEO YA UBUNIFU, MUDA NA UTULIVU MKUBWA

Licha ya kwamba uzuri wa kazi unahitaji sana ubora, umahiri na ubobevu wa mtaalamu anayeifanya lakini pia ubora, uzuri na umaridadi wa kazi unahitaji pia umakini, muda na utulivu mkubwa ambao unamsaidia mtu kutuliza akili na kupangilia mambo kwa usahihi na kwa kuzingatia kila kitu kinachochangia kwenye thamani husika.

UTULIVU NA UMAKINI UNAPUNGUZA SANA MAKOSA YA KIMPANGILIO NA KUPELEKEA KAZI KUWA NZURI NA YENYE UBORA

Hivyo kupata kitu cha thamani kunagharimu muda wenye umakini wa hali ya juu sambamba na utulivu ambao unagharimu sana umakini wa mtu, hasa ule muda makini.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *