UNAHITAJIKA USHIRIKIANO WA WATAALAMU WOTE WANAOHUSIKA KUJENGA MRADI HUSIKA TANGU MWANZO.

Ujenzi ni kati ya miradi ambayo kukamilika kwake huhusisha taaluma nyingi za fani mbalimbali katika utekelezaji wake. Fani hizi hutegemeana sana na kuwa na madhara mbalimbali pale mpangilio sahihi wa mtiririko wa utekelezaji wa mradi husika unapokosekana.

MIRADI YA UJENZI INAHUSISHA WATU WA FANI NYINGI

Tangu mwanzoni kabisa wa mradi watu wa fani zote husika wanapaswa kukutana na kuweka vikao ambapo kila mtu wa fani husika huja na ajenda zake za kile anachotegemea kufanikisha na atahitaji nini na wakati gani ili kumwezesha kufanya kazi yake kwa ubora na usahihi wa hali ya juu kabisa. Majadiliano maelewano na makubaliano na kisha ratiba kamili ya utekelezaji hupangiliwa na kila mtu kuwekwa katika nafasi ya kutekeleza majukumu yake kwa namna bora, rahisi na itakayoleta matokeo bora kabisa.

RATIBA YA UTEKELEZAJI WA UJENZI INAPASWA KUPANGILIWA BAADA YA VIKAO VYA MWANZO

Mambo yote yanayopaswa kutangulia yanapewa kipaumbele ambapo maandizi ya kiufundi na vifaa hutayarishwa kwa ajili ya kila mmoja kufanikisha kazi yake kwa wakati sahihi na kwa muda uliopangiliwa, endapo kuna muingiliano wa muda na majukumu inayoweza kupelekea kuchelewa au changamoto za utekelezaji jambo hili huzungumzwa na kutatuliwa na pande zote zinazohusika na kazi kuendelea.

CHANGAMOTO KUBWA ZILIZOZOELEKA HUZUNGUMZWA NA KUTATULIWA MWANZONI

Kwa utaratibu huu kazi nzima hufanyika kwa urahisi na kwa muda na kwa viwango vya juu bila majuto wala hasara ambayo iliweza kuepukika mwanzoni kutokana na kupangilia kila kitu kwa wakati.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *