KAMPUNI ZA UJENZI TANZANIA ZINAPASWA KUWA NA WASHAURI WA KITAALAMU.

Wote tunafahamu kwamba nchi yetu ina uhaba mkubwa sana linapokuja suala la washauri wa kitaalamu katika sekta mbalimbali. Sekta ya ujenzi ni kati ya maeneo ambayo washauri wa kitaalamu wamekuadimika sana kwenye miradi ya ujenzi, jambo linalopelekea kushuka sana kwa ubora na thamani ya miradi ya ujenzi ukilinganisha na thamani ya fedha iliyotumika kwenye miradi husika.

THAMANI YA JENGO INAPASWA KUENDANA NA FEDHA ILIYOTUMIKA

Kampuni nyingi za ujenzi Tanzania zinaendeshwa zaidi na wakandarasi wasio wataalamu wa fani za ujenzi pamoja na mafundi wenye uzoefu katika ufundi bila kuwa na wataalamu wenye uelewa mpana wa ujenzi kwa upande wa usanifu na uhandisi na hilo kupelekea makosa mengi ya wazi katika miradi mingi ya ujenzi Tanzania.

WATAALAMU WA USANIFU NA UHANDISI WANAHITAJIKA KATIKA KUHAKIKISHA UBORA NA THAMANI YA JENGO VINAFIKIWA

Ni jukumu la kila mmoja wetu kuanzia mamlaka husika, wakandarasi, wadau mbalimbali na hasa zaidi wateja wa miradi husika kuhakikisha mradi wowote unaojengwa unahusisha wataalamu katika kila hatua kwani mwisho wa mradi thamani itakayoongezwa na utaalamu husika itaonekana wazi.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

5 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *