GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA ZIKO TOFAUTI NA WENGI WANAVYOFIKIRI.

Kwenye suala linalohusisha fedha kila mtu huwa na mtazamo tofauti kutokana na mazoea na malezi aliyokuzwa nayo juu ya viwango mbalimbali vya fedha vinavyotajwa. Wakati mtu mwingine anaweza kuona milioni 50 kama ni fedha nyingi sana, mtu mwingine anaona milioni 200 kama ni fedha kidogo sana, na hiyo inatokana zaidi na malezi na mazoea pamoja na aina ya watu ambayo mhusika amejenga ukaribu nao. Jambo hilo limepelekea watu wengi na hasa vijana kutokana na kukosa uzoefu kwa mambo mengi kuwa na mtazamo wa tofauti kabisa linapokuja suala zima la gharama za ujenzi wa nyumba zao za kuishi.

WATU WENGI NA HASA VIJANA WANA MTAZAMO USIO SAHIHI JUU YA GHARAMA HALISI ZA UJENZI

Watu wengi kutokana na sababu niliyotaja hapa juu wamekuwa na mtazamo usio sahihi sana juu ya gharama za ujenzi ambapo unapomtajia gharama sahihi ya ujenzi anashangaa na kuhamaki na kutoamini kabisa kama anachosikia ni kweli. Kwa sababu yeye anaamini milioni 150 ni pesa nyingi sana pale unapomwambia nyumba hiyo itagharimu milioni 150 anashindwa kuamini na kuona kama pengine sio sahihi kwa sababu ya jinsi vile anavyoichukulia milioni 150.

MTAZAMO BINAFSI WA WATU JUU YA VIWANGO VYA FEDHA UMEKUWA UKIATHIRI SANA WATU KUKUBALIANA NA USAHIHI WA GHARAMA ZA UJENZI

Hivyo jambo la muhimu ni kwamba pale mtu anapotaka kufahamu gharama za ujenzi n ahata vitu vingine ni vyema kuweka mtazamo binafsi pembeni kwanza na kuiachia akili kuwa huru kukabiliana na uhalisia ili mtu upate ukweli na kujipanga kwa usahihi badala ya kujidanganya na kuja kukutana na ugumu pengine hata na majuto mbele ya safari.

UHALISIA WA GHARAMA HAUBADILIKI KUENDANA NA MTAZAMO BINAFSI WA MTU BALI MTU NDIYE ANABADILIKA

Hii ni kwa sababu gharama za ujenzi zitabaki katika uhalisia bila kujali mtazamo wa mtu yeyote iwe anaziona ni kubwa au hata yule anaziona ni ndogo, hakuna budi kukubaliana na uhalisia.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *