MASHARTI YA KIBALI CHA UJENZI YANATOFAUTIANA HALMASHAURI MOJA NA NYINGINE.

Halmashauri za majiji, manisapaa na miji ni taasisi zilipopewa mamlaka kisheria kwa ajili ya kusimamia mambo yote yanayotakiwa kusimamiwa na mamlaka ya kiserikali katika eneo husika. Halmashauri hizi mbalimbali nchini japo huwa na baadhi ya miongozi na mifumo inayoendana bado huwa hazifanani kwa kila kitu, kila halmashauri huwa na vikao vyake vya ndani ambavyo hupanga baadhi ya mambo kwa utofauti na hivyo vigezo na masharti ya kila halmashauri hutofautiana kwa kiasi.

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI

Ambapo kwa upande wa ujenzi unaweza kukuta kwa mfano wakati halmashauri ya manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam inahitaji mchoro wa kiwanja katika eneo linapojengwa nyumba kuwe na umbali wa mita 1.5 kutoka mpaka wa kiwanja mpaka nyumba inapoanzia, utakuta halmashauri ya jiji la Dodoma inataka umbali huo huo uwe wa mita 2 kutoka mpakani wa kiwanja mpaka nyumba inapoanzia.

HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA

Au unaweza kukuta kwa mfano wakati halmashauri ya manispaa ya Moshi inahitaji upeleke nakala tatu ngumu za seti 7 za michoro ya usanifu majengo na nakala mbili ngumu za seti 7 za michoro ya uhandisi mihimili, utakuta halmashauri ya jiji la Arusha wao wanahitaji upeleke nakala mbili ngumu za seti 7 za michoro ya usanifu wa majengo na nakala mbili ngumu za seti 7 za michoro ya uhandisi mihimili. Hali kadhalika kwa halmashauri nyingine hutofautiana vigezo na masharti haya hata kwenye idara nyingine kama afya, mazingira, mipango miji, n.k.,

HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI

Hivyo inahitaji mtu kufanya maandilizi mapema kwa kufuatilia vigezo masharti ya halmashauri husika badala ya kukariri kutoka kwenye uzoefu uliopata kutoka halmashauri nyingine.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *