KUPATA KIBALI CHA UJENZI UNAPASWA KUWA HUDAIWI KODI YA ARDHI.

Katika kufuatilia kibali cha ujenzi mara nyingi watu hukutana na usumbufu mwingi ikiwa hawajatimiza vigezo vyote vya kupewa kibali cha ujenzi. Ukiachana na changamoto za michoro kutokuwa imetimiza vigezo na masharti yote bado pia huwa kuna hati ya kiwanja inayoonyesha ukubwa wa kiwanja chenyewe, hadhi ya kiwanja na matumizi ya kiwanja ambavyo vyote vinapaswa pia kuwa vimetimiza vigezo na masharti ya kuendana na mradi husika.

Mbali na vigezo hivyo vya hati ya kiwanja halmashauri za majiji, manispaa na miji pia huangalia kama kiwanja husika kinadaiwa kodi yoyote ya ardhi kwa mwaka husika na miaka ya nyuma na ikiwa kiwanja hicho kina madeni ya nyuma ya kodi ya ardhi hutaweza kupewa kibali cha ujenzi kwa mradi husika mpaka umekamilisha kulipa kiasi chote cha kodi ambacho kiwanja chako kinadaiwa ndipo mchakato wa kuendelea kupitisha kibali cha ujenzi kwa mradi wako utaendelea.

MCHAKATO WA KUPATA KIBALI CHA UJENZI KWA MRADI WAKO UTAENDELEA BAADA YA KUWA HUDAIWI KODI YOYOTE YA ARDHI.

Hivyo ikiwa kuna madeni au malimbikizo ya kodi ya ardhi kwa miaka iliyopita ni muhimu sana ukayamaliza kwanza kabla hujapeleka ombi la kibali cha ujenzi kwani utazuiliwa kwanza mpaka umaliza kulipa madnei yote ya kodi ya ardhi ya miaka ya nyuma mpaka kufikia mwaka husika ndipo mchakato kupatiwa kibali cha ujenzi utaendelea.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *