MWISHO WA SIKU KATIKA UJENZI UTATHAMINI UBORA NA UTASAHAU GHARAMA.

Kwa kawaida binadamu huwa tunaongozwa na hisia katika maamuzi yote tunayofanya kwenye kila jambo na ndio maana mara nyingi utakuta tunakimbia maumivu ya namna yoyote ile ya kihisia na kukimbilia ahueni hata kama maumivu hayo ni hisia za hofu tu zisizo na uhalisia ndani yake wala madhara hasi kwetu. Jambo hili limepelekea tumekuwa tunafanya maamuzi ambayo huwa tunaishia kuyajutia baadaye na kuchukia kwa nini tulijiruhusu kuongozwa na hisia na kufanya maamuzi ambayo hayana maslahi na sisi zaidi ya kutuumiza wenyewe. Na hii ndio sababu watu hukimbilia zaidi vitu vya gharama nafuu hata kama unafuu huo ni kidogo sana ukilinganisha na thamani inayotolewa bila kujali ubora wa huduma au bidhaa husika kitu ambacho baada ya muda hujikuta katika majuto na kuona wazi kwamba ulipaswa kufanya maamuzi tofauti kwa sababu wakati wa majuto unakuta hata ile nafuu yenyewe imeshaongezeka na kuwa gharama kubwa kuliko hata ile gharama uliyoikimbia mwanzoni.

MAAMUZI BORA HULETA FURAHA NA UFAHARI BAADAYE JAPO HUWEZA KUHISI MAUMIVU MWANZONI

Sasa japo kwenye ujenzi watu huogopa sana gharama na kusahau kuhusu ubora mwisho wa siku hujikuta wakithamini zaidi ubora na kusahau kabisa kuhusu gharama, na ikiwa ubora umekuwa wa hovyo hata kama gharama ilikuwa nafuu basi hujikuta wakijuta sana kwa kuweka kipaumbele kwenye gharama na kusahau ubora. Hii ni kwa sababu gharama ni hisia kubwa za hofu zisizo na umuhimu mkubwa kama jinsi zinavyoonyesha kwa wakati huo ubora ambao ni muhimu zaidi ukiwa haukupi hofu za muda mfupi. Hivyo jambo la muhimu la kujifunza hapa ni kutafuta kuw amakini sana kwenye ubora wa huduma itakayopelekea kufurahia kazi yako kwa kipindi chote cha maisha yako ndio kisha baada ya kujihakikishia ubora ni wa viwango sahihi ndipo gharama iwe kipaumbele cha pili baada ya ubora. Kwa kufanya hivi utaepuka majuto na utafurahia na kujivunia maamuzi yako sahihi kwa kipindi kirefu sana.

GHARAMA NI HISIA ZA HOFU ZAIDI KULIKO UHALISIA AMBAZO KAMA HAKUNA BUSARA YA KUAMUA HUISHIA KWENYE MAJUTO

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *