CHANGAMOTO YA MAWE KWENYE ENEO LA UJENZI.

Inafahamika kwamba nyumba au jengo lolote linapaswa kuanzia chini kwenye msingi ili kuwa imara, na kina cha msingi ambacho jengo linatakiwa kufika inategemea na ukubwa au mzigo wa jengo husika ambao ardhi hiyo inaenda kubeba. Lakini pamoja na ulazima huo wa jengo kuanzia kwenye msingi kumekuwepo na changamoto kadhaa katika site husika za ujenzi zinazokuwa kikwazo kwa msingi husika kwenda chini sana. Ukiachana na changamoto ya kina cha maji ya ardhini kuwa juu sana kuna changamoto nyingine ya ardhi kuwa na mawe au miamba mikubwa ambayo haiwezi kuchimbika kiurahisi bila kutumia mashine kubwa zenye nguvu sana hasa baruti kubwa.

KUTUMIA BARUTI NA TINGATINGA KUVUNJA MIAMBA ILI KUJENGA MSINGI WA JENGO

Kwa kesi ya ardhi kuwa na mawe au miamba mikubwa na kushindwa kuchimbika hapa mtu unaweza kuamua kutumia njia mbili kuu. Moja ni kutumia baruti kulipua miamba hiyo ili ilainika na kuchimba kuiondoa kwa ajili ya kwenda chini zaidi kiasi ambacho msingi husika unahitajika kadiri ya mapendekeza ya mhandisi mtaalamu wa jengo husika. Na njia ya pili ni kutathimini miamba husika endapo ni imara kiasi cha kutosha kubeba jengo lenyewe kisha miamba yenyewe ndio kutumika kama msingi au sehemu ya msingi kutegemea na kiasi ambacho imefunika katika eneo la msingi husika.

KUJENGA JUU YA MIAMBA HUSIKA BAADA YA KUJIRIDHISHA UIMARA WAKE

Hii njia ya pili itapunguza kazi kubwa ya kujenga msingi na hata gharama yenyewe ya msingi na msingi mara nyingi unakuwa imara zaidi kuliko hata msingi wenyewe wa kujenga.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *