CHANGAMOTO YA KAZI YA UJENZI IKO KWENYE USIMAMIZI.

Udhaifu mkubwa tulionao katika kufikiri namna kazi mbalimbali zinafanyika huwa tunafikiria kiufundi zaidi lakini tunasahau suala zima la usimamizi. Hii ni sawa na mtu kufikiri kuwa jukumu la mzazi kwa mtoto ni kumpa chakula, mavazi na malazi na kupuuza suala la malezi kuwa halina maana ilimradi mtoto anakula, kuvaa na kulala. Unaweza kutafakari ni kiasi gani dhana hii ina upotofu ikiwa kuna mzazi anafikiri kwa mtazamo, unaweza kuona ni jinsi gani mtoto husika anaweza kuja kuharibika na kuwa wa hovyo kama huo ndio mtazamo wa mzazi wake.

USIMAMIZI SAHIHI KATIKA UJENZI NI JAMBO LISILOPEWA UZITO UNAOSTAHILI NA KUSABABISHA MIRADI MINGI YA UJENZI KUFANYIKI CHINI YA KIWANGO.

Sasa katika ujenzi napo mambo hayako tofauti sana, mtu kufikiri kwamba ujenzi ni ufundi peke yake na kupuuza swala la usimamizi ni dhana ambayo mara nyingi huja na gharama kubwa. Kwanza mradi husika utajiendea bila kuwa na ratiba maalum, pia mradi husika utakosa kuwa na viwango maalum ubora ambavyo vinasimamiwa ili kufikiwa na ufundi unaofanyika na kunaweza kujitokeza kurudiwa rudiwa kwa kazi itakayokuwa inaharibika kwa sababu hakuna mtu mwenye kuitazama kwa jicho la pembeni na ubaya zaidi jengo linaweza kujengwa kwa viwango vya chini vya ubora na hivyo kuhitaji ukarabati baada ya miaka michache baadaye.

USIMAMIZI KATIKA UJENZI NI KIPAUMBELE CHA KWANZA ILI MRADI UWE KATIKA VIWANGO SAHIHI VYA UBORA

Hivyo suala la usimamizi katika ujenzi linapaswa kupewa kipaumbele sana kwa sababu ndilo linaloamua mambo mengi katika ujenzi kuanzia muda wa kazi kukamilika, viwango vya ubora wa kazi husika, kusimamia kwa usahihi maamuzi yote ya kitaalamu yaliyoamuliwa na kuhakikisha kila kitu kinafanyika kama kilivyopangwa kila siku.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *