ITENDEE HAKI PESA YAKO KATIKA UJENZI KWA KUWEKA USIMAMIZI MAKINI

Kushindwa kufanya ujenzi wa viwango bora ni kushindwa tu kufikiria kwa usahihi, kwa maana nyingine ni kushindwa kujua nguvu kubwa uiweke wapi na wapi ili kupata huduma ya viwango bora na kufanikisha lengo kwa mafanikio ya hali ya juu. Moja kati ya vitu muhimu kabisa katika ujenzi ni ule ushauri wa kitaalamu kwenye mradi husika wa ujenzi, lakini kwa watu wengi kutojua kwa undani umuhimu huu wamekuwa wakishindwa kupata huduma bora na matokeo yake kujikuta wakikabiliana na makosa mengi kwa sababu ya viwango duni vya huduma za ujenzi wa mradi husika.

VIWANGO DUNI VYA HUDUMA ZA UJENZI VITAKULETEA HASARA KUBWA KULIKO GHARAMA AMBAYO UNGETUMIA KWENYE USIMAMIZI WA VIWANGO SAHIHI

Gharama ambayo mtu hutumia katika maeneo mengine ya mradi wa ujenzi hasa kwenye kununua vifaa vya ujenzi ni kubwa sana, tena utakuta mtu anahitaji kununua vifaa imara na bei ya juu ambavyo anaamini vina ubora wa kutosha lakini mtu huyo huyo utakuta anashindwa kuweka msimamizi wa kitaalamu wa viwango sahihi kama jinsi anavyochagua bidhaa zenye ubora katika mradi wake. Kuweka msimamizi wa viwango sahihi ni muhimu pengine kuliko hata vifaa vyenyewe kwani yeye ndiye anayeenda kusimamia utekelezaji wa vyote katika kufikia matokeo bora yanayotarajiwa. Kununua vifaa vya ujenzi vyenye ubora lakini ukashindwa kuajiri mtaalamu sahihi ni makosa makubwa sawa na kununua vyakula vibichi vizuri sana halafu vikapikwa na mtu asiyejua kupika, hapo unaweza kuona wazi kwamba gharama uliyotumia kununua vyakula vizuri ni kama umepata hasara tu.

GHARAMA ZA USIMAMIZI WA KITAALAMU NI NDOGO UKILINGANISHA NA GHARAMA NYINGINE ZA MRADI WA UJENZI

Uzuri ni kwamba gharama unayoitumia kwenye kuweka msimamizi sahihi wa mradi ndogo sana ukilinganisha na gharama nyingine za ujenzi hasa kwenye kununua vifaa. Hivyo ni maamuzi ya busara na akili kuhakikisha mradi wako unaoenda kutumia pesa nyingi sana kuufanikisha unaweka msimamizi wa viwango vya juu kabisa.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *