KUJIHAKIKISHIA UNAWEZA KUWA NA MFANO WA MCHORO WA RAMANI UNAOHITAJI.

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wateja kutamani aina fulani ya “design” ya nyumba ambayo imekuwa ikiwavutia kwa muda mrefu na kuwa na ndoto ya kuijenga pale wanapoanza ujenzi lakini inapofika wakati wa kutengeneza ramani wanashindwa kuieleza kwa usahihi kwa mtaalamu husika wa kuchora na hivyo inakuwa changamoto kuifanikisha. Hakuna “design” ambayo ni ngumu kiasi cha kushindwa kufanikishwa na mtaalamu wa kuchora ramani lakini changamoto hutokea kwenye maelewano kati ya mteja anayehitaji aina hiyo ya ramani kushindwa kuielezea kwa usahihi kwa mtaalamu husika na hivyo mtaalamu husika kwa kushindwa kumwelewa anafanya tofauti na malengo ya mteja husika.

NI RAHISI ZAIDI KUELEWEKA KWA UHAKIKA KUPITIA PICHA KULIKO MAELEZO

Njia nzuri, sahihi na ya uhakika ya kufanikisha unachotoka ni kuwa na mfano wa hiyo aina unayoihitaji, iwe ni ya paa au ya nyumba nzima aidha katika picha au mchoro wa mkono wa kile unachotaka. Kama utakuwa umeiona aina hiyo ya “design” mahali ulikopita unaweza kuangalia uwezekano wa kupiga picha au kufika hapo na mtaalamu husika ikiwa ni eneo linalofikika na kama ni mtandaoni basi unaweza kuipakua  na kumwonyesha au kumtumia mtaalamu husika kwamba hiyo ndio aina ya “design” unayohitaji, na mtaalamu husika atahakikisha unapata aina hiyo hiyo na hata ikitokea kuna mapungufu utakuwa na haki ya kumlaumu n ahata kumtaka arudie kwani ameona mwenyewe unachohitaji na hivyo analazimika kufanya hivyo.

MTALAAMU ATALAZIMIKA KUKUPA UNACHOTAKA KWANI ATAKUWA AMEKUELEWA KWA USAHIHI KABISA.

Hii ndio njia nzuri zaidi na rahisi kabisa ya kufanikisha hilo ikiwa maelezo hayawezi kujitosheleza kuweza kueleweka. Jambo la muhimu sana kuweka akili ni kwamba usimwingilie sana mtaalamu katika kazi yake, akishaelewa anachokwenda kufanya mwache afanye kwani kwa kumwingilia sana anaweza kuharibu ukashindwa kupata kile hasa unachohitaji.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *