SIO RAHISI KUJUA UJENZI WA VIWANGO BORA, TAFUTA MSIMAMIZI MAKINI AKUSAIDIE.

Jambo lolote la kitaalamu huwa na kanuni zake na viwango vyake ambavyo huweza kujulikana kwa usahihi na mtaalamu wa fani husika mwenye uzoefu mkubwa na muda mrefu, ambapo kadiri mtu anavyokuwa na uzoefu mkubwa na uwezo mkubwa katika taaluma husika ndivyo kadiri anavyokuwa kwenye nafasi ya kuweza kufanya vizuri zaidi na kusimamia kazi kwa viwango vya juu.

KUNA MAMBO MENGI YA KITAALAMU YANAYOHITAJI MTU MWENYE UWEZO MKUBWA KUYAONA NA KUYAFANYIA MAAMUZI SAHIHI

Mara nyingi sana tunapotembelea eneo la ujenzi lisilo na usimamizi makini na wa kitaalamu huwa tunakutana na changamoto mbalimbali ambazo zinatokana na kukosekana mtu mwenye uzoefu na mwenye kujua kwa hakika kitu sahihi cha kufanya. Katika makosa mengi mbalimbali yanayodunisha ubora wa jengo tunayokutana nayo, tatizo halipo tu kwenye makosa husika bali tatizo kubwa zaidi huwa ni wahusika kutojua hata kama hayo ni makosa. Kuanzia mteja anayejenga jengo husika mpaka watu aliowachagua kufanya nao kazi husika wote utakuta hakuna anayeona makosa hayo ya wazi yanayopunguza sana hadhi ya jengo kwa sababu ya kukosa usimamizi makini na sahihi kwa mradi husika.

KUNA MAMBO MENGI MUHIMU AMBAYO MTU ASIYE NA UTAALAMU PAMOJA UZOEFU MKUBWA HAWEZI KUYAONA

Hivyo ni vyema sana na muhimu kabisa unapoamua kufanya ujenzi wa jengo lako uhakikisha unaweka msimamizi mwenye utaalamu na uzoefu mkubwa ili aweze kukusaidia kuona makosa ambayo wewe binafsi sio rahisi kuyaona ambayo yanapunguza sana hadhi, ubora na uimara wa jengo lako.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *