PUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI KUENDANA NA BAJETI KWA KUMSHIRIKISHA MKADIRIAJI MAJENZI KATIKA KUANDAA MICHORO.
Mara kwa mara nimekuwa nikiwaambia watu mbalimbali kitu cha kwanza kinasababisha gharama za ujenzi kuwa kubwa ni ukubwa wa jengo lenyewe, yaani kadiri jengo na nafasi zake za ndani zinavyokuwa kubwa ndivyo gharama ya kulijenga inakuwa kubwa zaidi. Vitu vingine vinavyoongeza ukubwa wa gharama za ujenzi ni aina ya “design” na hasa urembo wa aina mbalimbali katika jengo pamoja na aina ya malighafi na vifaa vya ujenzi vinavyokwenda kutumika. Katika kupunguza gharama za vitu unapaswa kufuata njia sahihi za kufikia lengo hilo.
Kupunguza gharama za ujenzi kwa uhakika inapaswa kumshirikisha mkadiriaji majenzi au “Quantity Surveyor” mwanzoni kabisa kabla ya ramani kuanza kutengenezwa. Inapaswa kuweka kikao kati ya msanifu wa jengo, mteja pamoja na mkadiriaji majenzi na anaweza kuwepo mhandisi mihimili pia ambapo kutakuwa na mjadala mkubwa kati ya msanifu wa jengo ambaye atakuwa amekuja na mapendekezo ya namna jengo litakuwa kisha mkadiriaji majenzi ndiye atakuwa anajaribu kukosoa baadhi ya maeneo ambayo yanachukua gharama kubwa kisha utaangaliwa mbadala wa namna ya kupunguza au kuondoa kipengele husika kama hakina ulazima, ili mradi kazi nzima iweze kuendana na kiasi cha bajeti kilichoandaliwa japo mabadiliko hayo yanapaswa kuendana na uhalisia na sio tu kulazimisha kupunguza peke yake.
Baada ya kuandika upya mapendekezo yanayofikiwa kwenye kikao hiki ndipo kazi ya kuandaa ramani itaendelea na kabla ya mipango ya kuanza kujenga mradi husika.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!