GHARAMA ZA MAISHA ZA JENGO.

Mara zote tumekuwa tukizungumzia gharama za ujenzi wa jengo tangu mwanzoni wakati wa kutengeneza ramani mpaka jengo kukamilika kujengwa na kuhamia, hizo ndio gharama pekee za jengo ambazo zimekuwa zikizungumzwa mtu anapofikiria kuhusu gharama za nyumba. Ni sahihi kufikiria hivyo na kweli ndilo eneo ambalo gharama kubwa kabisa ya jengo inakwenda na huwa inahitajika ipatakine yote hata kama litajengwa kwa awamu lakini haliwezi kutumika kwa usahihi bila kukamilisha kujengwa hivyo kuhusisha gharama zote. Kukamilika kwa ujenzi ni kama kukamilisha jengo lakini kiuhalisia kuna gharama muhimu huwa tunazisahau linapokuja suala la maisha ya jengo ambazo ndio zitaamua thamani halisi ya jengo na hata faida yake kifedha hasa kama jengo ni la biashara, ambazo zinajulikana kama gharama za maisha za jengo.

MAKADIRIO YA GHARAMA ZA MAISHA ZA JENGO YANAKUPA PICHA HALISI YA GHARAMA ZA JENGO BAADA YA MATUMIZI

Gharama za maisha za jengo zinajumuisha zile gharama ambazo zitaendelea kutumika kuligharamia jengo katika kulifanyia ukarabati ili kuliweka katika hadhi yake na viwango vya juu vya ubora kila baada ya muda fulani kuhakikisha halipoteza mvuto wala thamani yake ambayo kwa kawaida huwa inapungua kila baada ya muda fulani kutokana na uchakavu na uharibifu. Gharama za maisha za jengo ni muhimu sana kujulikana mapema mwanzoni kabla ya kufanikisha michoro ya ramani kwani udhibiti wa gharama za maisha za jengo hufanyika kwa kudhibiti baadhi ya vipengele vya jengo vitakavyoongeza gharama tangu mwanzoni kabisa wakati wa kuandaa michoro ya ramani ya jengo husika.

KUJUA GHARAMA ZA MAISHA ZA JENGO KUTAONGEZA UMAKINI KATIKA MATUMIZI YA JENGO NA HATA KUFANYA UCHAGUZI SAHIHI WA MALIGHAFI

Gharama za maisha za jengo hufanyika kitaalamu na ni muhimu kushirikisha utaalamu wa ukadiriaji majenzi kwa ushirikiano na usanifu wa jengo, kwani kufahamu gharama za maisha za jengo kutasaidia kuweza kujua na kufanya udhibiti wenye manufaa makubwa kwako hasa kama jengo ni la biashara.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *