UBORA WA JENGO NI PAMOJA NA KUPUNGUZA SANA MATUMIZI YA NISHATI.

Tunapozungumzia ubora wa jengo/nyumba tumekuwa tukiangalia zaidi upande wa mwonekano, mpangilio wa kimatumizi wa ndani ya jengo, uhuru wa kimatumizi kadiri ya ukubwa wa vyumba, mandhari ya nje pamoja na uimara wa mihimili wa jengo lenyewe. Lakini kuna vitu muhimu sana tunavisahau ambavyo vian mchango chanya kwenye kuliongezea jengo ubora. Matumizi ya nishati ni moja ya vitu muhimu sana katika jengo kwani yanaongeza gharama za uendeshaji wa jengo kwa kiasi kikubwa sana hivyo yanakuwa sehemu muhimu sana ya kuamua thamani ya jengo husika na ubora wake.

UWAZI MKUBWA UNARUHUSU MWANGA NA HEWA VYA KUTOSHA BILA KUTEGEMEA MATUMIZI YA NISHATI

Jengo lolote ambalo linahesabiwa kuwa ni jengo bora linatakiwa kupunguza sana matumizi ya nishati kwa kutegemea mifumo ya asili zaidi ya kuingiza mwanga na hewa ndani ya jengo kadiri ya mazingira ya eneo husika. Kwa mfano kama jengo ni kubwa sana na baadhi ya nafasi ndani ya jengo kama vile vyumba zinakosa kuwa na maeneo ya kupitisha mwanga wa kutosha italazimu kuweka madirisha makubwa sana upande wa uso wa chumba hali kadhalika na hewa pia, au ili kuleta mwanga na hewa katika jengo la namna hii kunakuwepo na eneo la wazi katikati ya jengo ambalo halina paa kwa juu litakaloruhusu mwanga na hewa unaotoka juu kuingia ndani ya jengo kwa vyumba ambavyo viko ndani na havionekani kwa upande wan je. Mwanga na hewa asili vinavyopaswa kuwa ni vya kutosha katika kila eneo la ndani ya jengo ili kupunguza matumizi ya nishati hasa wakati wa mchana ambapo kuna mwanga wa kutosha na wakati mwingine joto pia kwa maeneo yenye joto. Japo mifumo ya mwanga na hewa itawekwa ndani ya jengo lakini inaweza kutumika kwa kiasi kidogo kadiri inavyowezekana pale inapolazimu lakini muda mwingi jengo linapaswa kupunguza sana matumizi ya nishati ili kupunguza gharama za uendeshaji wa jengo na hata kuchangia katika kutunza mazingira.

UBUNIFU WA KISANIFU NDIO HUFANYA KAZI YA KUHAKIKISHA JENGO LINAPUNGUZA MATUMIZI YA NISHATI KWA KIASI KIKUBWA VYA KUTOSHA

Sehemu kubwa ya kufanikisha hili ipo kwa msanifu majengo ambaye kutokana na mpangilio sahihi wa jengo kimatumizi na hata baadhi ya vipengele vya jengo ndio hupelekea jengo kupunguza sana matumizi ya nishati.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *