MAELEWANO KATI YA MTAALAMU WA KUFANYA MICHORO NA MKANDARASI.

Namna kazi nyingi za ujenzi zimekuwa zikifanyika na mwenendo wake unavyokuwa kuna miradi mingi ambayo ushirikiano kati ya mtaaamu wa kufanya michoro au msanifu majengo na mkandarasi anaeenda kutekeleza mradi husika unakuwa haupo kabisa, wakati mwingine hawafahamiana kabisa au hawajawahi kuwasiliana. Jambo hili limekuwa linasababisha changamoto kadhaa wakati wa ujenzi wakati mwingine hata na lawama nyingi kwa mhusika ambaye pengine angeweza kutoa maelezo akaeleweka au kufanya marekebisho yatakayoendana na mtazamo mpya kadiri ya mazingira husika na uelewa wa wanaotekeleza mradi wenyewe.

MTAALAMU ANAWEZA KUELEZEA KWA USAHIHI MICHORO ALIYOIFANYA LAKINI ANAPOKOSEKANA KABISA HUWEZI KUFIKIRIWA ALIKOSEA SANA

Kimsingi kabisa kuna umuhimu mkubwa au naweza kusema ulazima wa mtaalamu anayefanya michoro kuwa karibu na mkandarasi anayejenga mwanzoni kabisa wakati wa kuandaa michoro, lugha ziwe zinaendana na hata baada ya kutoa michoro ya mwanzo ya mapendekezo ijadiliwe kwa ushirikiano kati ya mtaalamu wa kuandaa michoro, mkandarasi na mteja. Hili litasaidia kujadili changamoto na maeneo yote yenye utata sambamba hata na gharama za ufundi, muda wa kukamilisha mradi n ahata mahitaji muhimu ambayo upatikanaji wake unaweza kuchukua muda mrefu au kuwa changamoto. Wakati mwingine pia mtaalamu anayeandaa michoro kama hana uzoefu mkubwa na ujenzi huweza kufanya michoro aidha ambayo haiku katika uhalisia kwa maana ya migumu kujengeka kwa teknolojia inayoweza kupatikana au kujengeka katika viwango duni na kushindwa kufanikisha kupata ule mwonekano ambao ulivutia sana mwanzoni, wakati mwingine mkandarasi au fundi husika akawa hana tu uwezo wa kufanya hiyo kazi kwa sababu hana uzoefu wa kutosha hivyo akatafutwa mwingine.

CHANGAMOTO ZA MICHORO HUWA NYINGI NA ZENYE MADHARA MAKUBWA, USHIRIKIANO MKUBWA HUHITAJIKA ILI KURAHISISHA MAMBO

Zoezi zima la utekelezaji wa mradi husika wa ujenzi litakuwa rahisi na hata kutumia muda mchache zaidi na kupunguza makosa kwa kiasi kikubwa kutakapokuwa na ushirikiano huu kati ya mtaalamu anayeandaa michoro na mkandarasi anayejenga.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *