KUPATA KIVULI CHA UHAKIKA PANDA MITI YA KIVULI.

Katika maeneo mbalimbali tunayojenga nyumba zetu tumekuwa tukikutana na changamoto ya mwanga wa jua unaingia mpaka ndani ya vyumba unaoumiza watumiaji wa jengo hasa nyakati za asubuhi na jioni. Kitaalamu hili mara nyingi tumekuwa tukijaribu kulitatua kwa kutafuta uelekeo jengo ambao utakuwa sahihi zaidi kuepuka miale ya jua kugonga moja kwa moja mpaka ndani, lakini changamoto ya njia hii ni kwamba unapojaribu kugeuza uelekeo wa jengo ili eneo moja lisiathirike maana yake moja kwa moja eneo lingine linaenda kuathirika ambalo utakuwa umehamishia huo upande kwenye jua, na bado hata unaweza kuhamisha eneo lisiathirike kwa jua la asubuhi lakini likaja kuathririka na jua la jioni. Hivyo njia bado ina changamoto nyingi kwani utakwepesha upande mmoja huku ukiumiza upande mwingine wa jengo labda unaiokoa sebule huku ukiliumiza jiko au unaokoa chumba kikubwa huku ukiumiza chumba kidogo.

KUTUMIA “SHADING DEVICES” HUWEZA KUHARIBU MUONEKANO WA JENGO.

Suluhisho lingine kitaalamu hutumika kuweka vifaa vya kuleta kivuli vinavyowekwa pembezoni kwenye maeneo yenye uwazi maarufu kama “shading devices”, vifaa hivi hutokeza kwa nje ili kuzuia miale ya jua isiingie sana ndani badala yake iishie mwanzoni mwa uwazi husika bila kuathiri waliopo ndani au mbadala wake huwekwa ukuta mpana ambapo dirisha linaingia ndani sana hivyo miale inaishia mwanzoni mwa dirisha bila kuathiri waliopo ndani. Njia inafanya kazi kwa kiasi kikubwa lakini changamoto yake ni kwamba mara nyingi ina gharama zaidi na pia inaweza kuharibu mwonekano wa jengo kwa namna ambayo ni tofauti na inavyotarajiwa na wengi.

HAIWEZEKANI KULIZUIA JUA MOJA KWA MOJA, BILA KUUMIZA UPANDE MWINGINE LICHA PIA YA JUA KUKULAZIMISHA UELEKEO PENGINE USIOUTAKA

Hivyo sasa, kuepuka changamoto na vikwazo vya namna hii huku ukifanikisha kupata kivuli cha kutosha ambacho kitafanya jango lote kuepuka adha ya kuumizwa na miale ya jua hasa nyakati za asubuhi na jioni ni kupanda miti ya kivuli itakayoweza kulilinda jengo.

MITI YA KIVULI ITALILINDA JENGO SAMBAMBA NA KUBORESHA SANA MAZINGIRA YA ENEO HUSIKA

Utahitaji ubunifu mzuri sana wa kimpangilio wa namna ya kutengeneza bustani na miti kwa namna ambayo itakuwa sahihi sana kadiri ya mpangilio na mwelekeo wa jengo pamoja na asili ya jiografia ya eneo husika.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *