MSIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI ANAPASWA KUWA NA ORODHA YA MAMBO ANAYOFANYIA KAZI
Ujenzi ni kazi inayohusisha vitu vingi sana katika utekelezaji wake, jambo hili unaweza kuliona ukiwa kama mtaalamu wa ushauri wa ujenzi, mkandarasi au mteja unayefanya ujenzi unapokuwa unatembelea mradi wa ujenzi. Utakuta kuna vitu vingi sana vya kutekeleza ambavyo pia vinahitaji kumbukumbu na umakini wa hali ya juu sana katika utekelezaji wake na ambavyo mara nyingi huwa vinasahaulika au kukumbukwa kwa kuchelewa na hivyo vinapelekea hasara ya kubomoa na kurudia kazi au kubaki na kazi iliyojengwa chini ya kiwango kwa sababu ya kusahaulika kwa baadhi ya mambo ya msingi.
Hivyo, kwa maana hii msimamizi wa kazi ya ujenzi anapaswa kuwa na orodha ya mambo yote yanayosubiri kuingizwa katika utekelezaji na kila linapotokea jambo jipya la kutekelezwa linapaswa kuongezwa kwenye orodha hii ya mambo ya kutekeleza. Orodha hii sio tu itatakiwa kuwa na orodha ya mambo ya kutekeleza bali pia viwango vya ubora vinavyopaswa kufikiwa na hivyo msimamizi au mkaguzi mkuu anatakiwa kukagua matokeo yanayotarajiwa kufikiwa bila kupokea sababu yoyote kwani ni jukumu la msimamizi wa mradi kuhakikisha matokeo husika yanafikiwa. Kwa kutumia orodhas ya mambo ya kutekeleza mradi unakuwa kwenye nafasi ya kufanikiwa kwa usahihi na kwa haraka na katika viwango bora kabisa vilivyopangwa.
Jukumu la kutengeneza orodha ya vitu husika inapaswa kuandaliwa na mtaalamu mkuu wa ushauri wa kitaalamu wa mradi akishirikiana kwa karibu na wakandarasi wa mradi husika.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!