MAAMUZI YOTE YA NAMNA UJENZI UTAFANYIKA YAFANYIKE MWANZONI.

Katika ujenzi vitu vingi vinavyofanyika katika kila kipengele mara nyingi huwa na uhusiano na vitu vingine ambpo inaweza kuwa ni uhusiano wa kiujenzi, kigharama au kimpangilio lakini mwisho wa siku maamuzi ya namna ya kujenga kipengele kimoja mara nyingi huwa na madhara kwa vipengele vingine kwa namna moja au nyingine. Kutokana na kazi nyingi kufanyika bila kuweka umakini kwenye mpangilio mzima kulingana na uhusiano imekuwa ni changamoto ambayo imekuwa ikigharimu miradi mingi kuanzia gharama, usumbufu, muda na hata ubora wa kazi.

MAAMUZI SAHIHI YANAPASWA KUANZIA MWANZONI KABISA MWA MRADI WA UJENZI.

Hivyo ni muhimu sana pande zote zinahusika na mradi husika wa ujenzi kukaa chini mwanzoni na kjadili kila kipengele katika mradi mzima kuanzia kwenye msingi mpaka umaliziaji wa mwisho na kuhamia na mpangilio wa thamani za ndani mpaka matumizi yenyewe ya jengo hasa kwenye eneo la mzunguko wa ndani. Kila kitu kikiwa kimeamuliwa mwanzoni mwa mradi itapelekea ufanyaji wa maamuzi sahihi katika kila hatua na kurahisha sana utekelezaji wa mradi husika na hata kuokoa muda, gharama, usumbufu na kuzingatia ubora wa kazi.

MAAMUZI SAHIHI YA MWANZONI LAZIMA YAHUSISHE PANDE ZOTE ZINAZOHUSIKA KWENYE KUAMUA KUHUSU MRADI HUSIKA

Maamuzi haya yanapaswa kuhusisha pande kuu tatu ambazo ni utengenezaji wa michoro ya ramani, ujenzi wenyewe pamoja na upande wa mteja na yanapaswa kufanyika mwanzoni kabisa wakati wa kuanza kutengeneza ramani na ikiwa ramani ipo tayari basi mapema sana kabla ujenzi haujaanza katika hatua ya msingi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *