TIMIZA VIGEZO VYA MAMLAKA ZA UJENZI KUEPUKA KUSHAWISHIWA AU KUSHAWISHIKA KUTOA RUSHWA.

Kuna watu wengi ambao sio waumini wa kutoa rushwa na wengine hawako tayari kabisa kutoa rushwa hata kama changamoto ni kubwa kiasi gani watajaribu kutafuta njia mbadala kwa sababu kutoa rushwa kwao ni kinyume na sheria zao binafsi za kimaadili na hivyo hawako tayari kuvunja sheria hizo. Lakini watu kwa sababu ya mazoezi na tabia zilizojijenga miongoni mwetu na kwenye mifumo wamekuwa wakiamini kwamba haiwezekani kufanikisha kupata kibali cha ujenzi bila kutoa rushwa endapo wale wenye mamlaka ya kukuruhusu wanahitaji uwape rushwa kwanza ndio wakuruhusu kuendelea. Japo ni kweli kwamba wakati mwingine unaweza kuzungushwa sana ikiwa watu wanahitaji uwape kitu fulani lakini mara nyingi kama sio mar azote huwa wanatafuta kwanzaeneo lenye udhaifu.

FIKA KWENYE OFISI ZA MAMLAKA HUSIKA KUPEWA MAELEKEZO KABLA YA KUPELEKA SAHIHI NYARAKA KWA AJILI YA KUPATA KIBALI

Ikiwa unataka kuepuka kutoa rushwa hatua ya kwanza kabisa ni kuhakikisha umefuata sheria zote zilizowekwa na mamlaka na umezingatia masharti na vigezo vyao. Namna sahihi ya kuweza kufahamu jinsi ya unaweza kufahamu vigezo hivi ni kutafuta mtaalamu wa usanifu na uhandisi wa majengo na kwenda kuonana na watu wa mamlaka husika, tena ambao wako kwenye kitengo husika kwa wakati huo kisha kuzungumza nao kuweza kufahamu kila kitu kinachohitajika na changamoto ambazo huwakabili watu wanaoshindwa kufikia vigezo na kuzuiliwa kisha kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, vigezo na masharti ya mamlaka husika. Kwa kufanya hivi itasaidia kwanza kufahamu kwa undani kwamba matatizo haswa huwa yanatokea eneo gani lakini pia utakuwa umeonana na wahusika wakakupa vigezo na masharti wenyewe ambavyo umevitimiza kama walivyokueleza hivyo unapopelekea michoro iliyofuata ushauri wao na mahitaji yao watakuwa hawana namna ya kufanya zaidi ya kukupatia kibali kwani vyote walivyokueleza ndivyo ulivyoenda kufanya. Lakini inapotokea bado wanaleta ubishi unaweza kuendelea kufuatilia na kuhitaji kujua wapi pengine pa kubadili na mwisho watakosa visingizio na kukuona wewe ni wa tofauti na huhitaji upendeleo wa aina yoyote ile hivyo watajkuta wanakosa sababu ya kukuzuia na mwisho watakupatia.

KAMA IMANI YAKO NA MAADILI BINAFSI HAYAKURUSU KUTOA RUSHWA BADO UNA NAFASI YA KUTAFUTA NJIA MBADALA

Muhimu cha kukumbuka ni kwamba kushawishiwa au kushawishika kutoa rushwa siku zote kunaanzia kwenye udhaifu wowote ulio upande wake katika nyaraka unazojaribu kutumia kuombea kibali cha ujenzi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *