USIKUBALI KUJENGA JENGO LENYE MUONEKANO WA HOVYO KWA ZAMA HIZI.

Uzuri wa muonekano wa nyumba/jengo ni sehemu muhimu sana ya mradi wa ujenzi na pia unachangia sana katika kuongeza ubora na thamani ya jengo husika. Ni wazi kwamba jengo linalovutia litapendwa zaidi na watu na watakuwa tayari kulipa gharama zaidi kwa huduma watakayoipata kwenye jengo husika iwe ni kupanga kwa ajili ya makazi, biashara au hata katika kulinunua. Ikiwa jengo ni la binafsi kwa matumizi ya makazi binafsi uzuri wa kimuonekano wa jengo unaleta kuridhika sana na kuifurahia nyumba kila unapoiangilia na kuleta kuridhika kwa kiasi kikubwa na kuimarisha afya ya akili na kwa kuwa jengo ni kitu kinachodumu kwa miaka mingi sana basi ukifanya kazi nzuri itakupa kuifurahia kila siku kwa miaka mingi sana lakini kazi mbaya itakuletea kusononeka pia kwa miaka mingi sana.

JENGO LENYE KUVUTIA HUHAMASISHA KILA MTU NA HUONEKANA NI LENYE THAMANI ZAIDI

Jengo zuri husifiwa sana pia na watu na huonekana ni sehemu ya umakini wa mmiliki wa nyumba/jengo husika jambo ambalo huchangia mtu kuheshimiwa zaidi na watu wa karibu kama vile wa familia na watu wa mbali pia. Katika zama tunazoishi sasa mtu kushindwa kuwa na jengo zuri na bora kadiri unavyotamani mwenyewe ni ujinga na uzembe. Kwanza kabisa unaweza kupata watu sahihi wa kukufanyia kazi nzuri sana kadiri unavyotaka wewe na pia gharama ya kufanyiwa kazi nzuri ni kiasi kidogo sana ambacho kinaweza kuwa takariban asilimia 1% ya gharama ya kujenga jengo lote mpaka kukamilika, lakini huku ikiongeza thamani ya jengo kwa kiasi kikubwa sana na kutoa mwongozo sahihi wa namna ya kufanikisha kazi kwa viwango vya ubora wa hali ya juu. Gharama hii ni kidogo sana ukijaribu kulinganisha na miaka ambayo watu watakuwa wakilitazama jengo na kulihukumu kulingana na mwonekano wake kitu ambacho ndio kinaamua thamani yake pia.

KUFANYA KAZI NA WATAALAMU WENYE UWEZO NA UZOEFU ITASAIDIA KUFANIKISHA KUTIMIZA KILE UNACHOKITAKA KWA UHAKIKA ZAIDI

Jambo la muhimu na la msingi kabisa ni kuhakikisha kwamba unafanya kazi na mtaalamu mwenye uwezo mkubwa vya kutosha kutengeneza jengo lenye viwango vya juu vya ubora na uzuri wa mwonekano kupata kile hasa unachotaka au ambacho ni bora sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *