MAENEO 9 YA USIMAMIZI KATIKA USIMAMIZI WA JUMLA WA MRADI WA UJENZI(PROJECT MANAGEMENT)

Wote tunakubaliana kwamba shughuli yoyote ya ujenzi inaweza kufanyika kwa viwango vya juu vya ubora au kwa viwango vya chini vya ubora kutegemeana na uwezo wa kiusimamizi(project management). Sasa usimamizi sahihi na kamili wa ujenzi unahusisha maeneo haya tisa.

  1. Usimamizi wa kuunganisha shughuli zote za ujenzi ziende katika utaratibu sahihi uliopangwa kwa ajili ya kufanikisha matokeo tarajiwa, kwa mfano kuhakikisha kwamba shughuli zote zinaendana na muda uliopangwa na zinafanyika kwa kadiri zinavyotegemeana.

2. Usimamizi wa ukubwa wa mradi, huu ni usimamizi unaohusisha kujua mradi wa ujenzi ni mkubwa kiasi gani na utafanyika kwa namna gani ambayo itapelekea kukamilika kama ilivyopangwa(Project scope).

3. Usimamizi wa muda katika mradi wa ujenzi, huu ni usimamizi wa mradi wa ujenzi unaohakikisha kila kitu kinafanyika katika muda uliopangwa na mradi kumalizika ndani ya muda uliopangwa.

4. Usimamizi wa gharama katika mradi wa ujenzi, huu ni usimamizi wa mradi wa ujenzi ambao unahakikisha kwamba mradi unakamilika ndani ya bajeti ya kiasi cha fedha kilichopangwa.

USIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI NI MCHAKATO MPANA

5. Usimamizi wa ubora katika mardi wa ujenzi, huu ni usimamizi wa ujenzi ambao unaohakikisha kwamba mradi unafanyika katika viwango vya juu vya ubora vilivyopangwa kwa kuhakikisha kila rasilimali inayohitajika kufanikisha hilo inapatikana kwa muda sahihi.

6. Usimamizi wa rasilimali watu katika mradi wa ujenzi, huu ni usimamizi wa mradi wa ujenzi unaohakikisha kwamba watalaamu wote wanaohusika katika ujenzi wanapatikana ambao wana uwezo wa kutosha kufanikisha mradi husika katika viwango vinavyotarajiwa.

7. Usimamizi wa mawasiliano katika mradi wa ujenzi, huu ni usimamizi wa mradi wa ujenzi unaohakikisha kwamba taarifa sahihi zinawafikia watu kwa wakati sahihi kadiri inavyohitajika.

8. Usimamizi wa hatari zinaweza kujitokeza katika mradi wa ujenzi, huu ni usimamizi wa mradi wa ujenzi unaohusisha kuzifuatilia na kuzifahamu hatari zote zinazoweza kujitokeza katika mradi wa ujenzi na kujiandaa kukabiliana nazo muda wowote zitakapotokea.

9. Usimamzi wa wakandarasi wadogo wanaoajiriwa na mkandarasi mkuu katika mradi wa ujenzi, huu ni usimamizi unaohusisha kuwafuatilia na kufuatilia kazi za wakandarasi wadogo kwenye mradi wa ujenzi kuhakikisha zinafanyika katika utaratibu uliopangwa na unaokubalika.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *