ATHARI ZA KIMAZINGIRA ZA MRADI WA UJENZI.

Mradi wowote wa ujenzi huja na athari zake kimazingira kulingana na aina ya mradi husika. Athari zinatofautiana viwangoa mabpo kuna miradi mingine huja na athari hasi kidogo sana na mingine huja na athari hasi nyingi zaidi na kadiri mradi unapokuwa na athari nyingi sana hasi ndivyo kadiri unavyozidi kupoteza uhalali wa kuwa katika eneo husika kwa mujibu wa sheria na taratibu za udhibiti wa athari za miradi mbalimbali kimazingira. Athari hasi hizi zinaweza kuwa katika namna nyingi kama vile uchafuzi wa kimazingira wa ardhi, vyanzo vya maji, hewa au sauti ya mahali ambapo uchafuzi huu unategemea na matumizi ya mradi husika. Suala la athari za kimazingira za mradi wa ujenzi ni nyeti sana kwa sababu linaathiri moja kwa moja watu wanaoishi katika eneo husika uliopo mradi wa ujenzi na hivyo hasa miradi mikubwa huweza kukutana na changamoto nyingi za kupata uhalali wa kujengwa kutokana kwa wanaharakati wa kimazingira wakishirikiana kwa karibu na mamlaka husika.

MRADI MKUBWA NI RAHISI KUKWAMISHWA NA WANAHARAKATI WA KIMAZINGIRA KAMA HUTACHUKUA TAHADHARI MAPEMA

Hasa kwa miradi mikubwa ikiwa unahitaji kujua namna ya kukabiliana na athari za kimazingira za mradi wa ujenzi unaotegemea kujengwa katika eneo fulani utahitaji kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa masuala ya mazingira. Wataalamu watakaofanya utafiti wa kimazingira kwa eneo husika na kukuletea taarifa ya endapo mradi huo unaweza kufanikiwa au kupata vizuizi kutoka kwa watu wa mazingira. Ikiwa utaona mradi utakutana na vizuizi kutokana na athari kubwa za kimazingira zitakazoletwa na mradi husika unaweza kupata ushauri kutoka kwa wataalamu hao hao wa nini cha kufanya ili mradi uweze kuondokana na vikwazo hivyo vya kimazingira. Wataalamu hawa wa mazingira (environmental consultants) watakupa ushauri sahihi wa nini uepuke na kupunguza ili kuepuka vikwazo hivyo. Mwisho wataalamu hawa watakutengenezea ripoti sahihi ya kimazingira kadiri walivyokushauri ambayo itaweza kupitishwa kwamba eneo hilo linafaa kwa mradi husika na hivyo utaweza kuendelea na mradi wa ujenzi bila vipingamizi.

KUFAHAMU UIMARA NA UDHAIFU WAKO KIMAZINGIRA MAPEMA ITAKUSAIDIA SANA KUEPUKA VIKWAZO NA VIPINGAMIZI KUTOKA KWENYE MAMLAKA HUSIKA

Ni muhimu sana hasa pale unapofikiria kuhusu mradi mkubwa wa ujenzi kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa kimazingira kwa sababu ukienda moja kwa moja mradi ukaanza kukutana na vikwazo inaweza kuja kuwa changamoto baadaye kuwashawishi mamlaka husika kwamba mradi wako ni salama dhidi ya athari za kimazingira.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *