KWA MRADI WA UJENZI UNAOENDESHWA BILA KUFUATA UTARATIBU ULIOWEKWA NA MAMLAKA HUSIKA KISHERIA INAPASWA AWEPO MTU WA KUFANYA MAAMUZI YA MWISHO.

Wote tunajua kwamba mamlaka za ujenzi zimeweka utaratibu unaotakiwa kufuatwa katika miradi ya ujenzi mpaka kufikia mtu mwenye maamuzi ya mwisho kabisa katika ujenzi pale inapokuwa inatakiwa. Kwa kawaida maamuzi mengi ya ujenzi na hasa ya kitaalamu hufanywa na mshauri wa kitaalamu wa eneo husika(consultancy) na kama hayupo basi atafanya msaidizi wake au mtu mwingine yeyote anayefuata mwenye uelewa mpana zaidi kwenye kazi za ushauri wa kitaalamu. Wote tunajua kwamba jambo hili liko kisheria na halihitaji mjadala wala mivutano kwani mwisho wa siku kila mtu atawajibika kisheria kadiri ya nafasi aliyokuwepo na hakuna mtu atakubali kubeba mzigo wa mwingine kwa kufanya maamuzi yasiyo sahihi ili kumfurahisha mwingine.

Lakini kwenye miradi isiyofuata utaratibu wa kisheria mara nyingi mambo huweza kuwa tofauti sana ambapo maamuzi huweza kufanywa na mtu yeyote na mwingine kupingana nayo kitu ambacho japo ni kizuri katika kufahamu udhaifu na uimara wa pande zote lakini kisipoambatana na busara ya kimaamuzi huwezi kupelekea mivutano isiyoisha. Hivyo ni muhimu na vyema kabisa kwa miradi ambayo haiendeshwi kwa mujibu wa taratibu za kisheria zilizopangwa na mamlaka husika au hata kama inafuata taratibu hizo lakini kuna uhuru mkubwa wa kutoa amani ili kufanya maamuzi sahihi zaidi, ni muhimu mwisho wa siku akawepo mtu wa kufanya maamuzi ya mwisho ambayo ndio yatakayofuatwa pale ambapo mjadala umeshindwa kufikia tamati kwa sababu zozote zile. Jambo hili litasaidia kujua kwanza ni nani anayewajibika kwa maamuzi kufanyika kwa namna yatakavyofanyika na nani wa kuangaliwa pale panapotokea mivutano isiyoisha.

Kuwepo kwa mwamuzi wa mwisho ambaye mara nyingi atatakiwa kuwa mshauri wa kitaalamu mwenye uzoefu kutaepusha migongano itakayoweza kuchelewesha kazi sambamba na kutoelewana kunakoweza kuathiri ubora wa mradi wa ujenzi husika.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *