KATIKA UJENZI BORA, GHARAMA ISIWE KIKWAZO.

Katika ujenzi karibu mara zote makosa huwa yanatokea ambapo inategemea endapo hakutakuwa na ukaguzi wa mara kwa mara makosa huweza kuwa mengi na gharama ya kuyarekebisha kuwa kubwa lakini kunapokuwepo na ufuatiliaji wa karibu wa mara kwa mara makosa hupungua na gharama ya kuyarekebisha kupungua pia. Ni muhimu sana kuwepo kwa mtaalamu wa kufanya ukaguzi huru mara kwa mara kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa usahihi na kwa ubora wa hali ya juu na kuleta mrejesho mapema pale ambapo makosa yanafanyika.

MAKOSA YANAPOGUNDULIKA MAPEMA INAPUNGUZA SANA GHARAMA YA KUYAREKEBISHA

Makosa ya kiufundi na kisanifu yanapofanyika mara nyingi huhitaji gharama za ziada kuyerekebisha, gharama ambazo kama utaratibu sahihi haujawekwa wazi huwa hazieleweki kwamba zinabebwa na nani na hivyo kila upande unakaa kimya. Upande wa mjenzi/mkandarasi mara nyingi hukaa kimya au hata kujaribu kufunika tatizo au kulitetea ionekano sio kosa kubwa au sio kosa kabisa ili kukwepa kubeba mzigo wa gharama ambazo ziko nje ya bajeti yake. Upande wa mteja hutegemea kwamba kwa sababu kosa limefanywa na mjenzi mwenyewe basi ni jukumu lake kulirekebisha kwa sababu ni kosa lake. Jambo hili limekuwa chanzo cha kazi nyingi kubaki na makossa licha ya kwamba gharama hizi huwa ndogo sana ukilinganisha na thamani ya jengo kwa ujumla hasa kama tatizo husika halijachelewa kutokana na ukaguzi wa mara kwa mara. Kwa maana hii ni muhimu sana kwa mteja n ahata mjenzi kufahamu udhaifu huu na kulijadili hili mapema kwa faida ya pande zote.

MKAGUZI AMBAYE NI MSHAURI WA KITAALAMU ATASAIDIA SANA KUHAKIKISHA UBORA KWA KUPUNGUZA MAKOSA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.

Ni muhimu sana mteja kuweka msimamizi ambaye ni mshauri wa kitaalamu wa kuhakikisha anafanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na kurudisha mrejesho na ikiwa kuna makosa yamefanyika yarekebishwe mapema kwa gharama ndogo kabla hayajafikia kuwa changamoto kubwa. Hili litahakikisha kwamba jengo linajengwa katika viwango sahihi hivyo kuepuka majuto ya siku za mbele wakati wa kulitumia jengo.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *