UTAALAMU SAHIHI NA UZOEFU KWENYE UJENZI NI KIPAUMBELE CHA KWANZA KATIKA KUFIKIA UBORA.

Tunapozungumzia ubora hasa kwenye nchi za Ulimwengu wa tatu huwa ni vigumu kidogo mtu kueleweka kutokana na mazoea na tabia ambazo watu tayari wamejijengea. Kutokana na udhaifu wa kuongozwa na hisia watu wameacha kabisa kujali kuhusu ubora wa vitu na badala yake wamekuwa wakiangalia gharama ya vitu peke yake na eneo wanalofeli sana ni kusahau kwamba kitu chenye gharama nafuu kuliko vyote mara nyingi sio bora. Hapa sijaribu kumwambia mtu asitatfute kitu chenye unafuu ila nasisitiza kwamba kipaumbele cha kwanza katika huduma yoyote unayotafuta kiwe ni ubora kabla ya gharama, yaani ubora uitangulie gharama na sio kinyume chake. Hii ni kwa sababu ni ubora ufeli kwenye gharama kuliko ufeli kwenye ubora kwa sababu hakuna kitu chenye gharama kubwa duniani kama kitu kilichokosa ubora. Ukifeli kwenye ubora mara nyingi huishia kwenye hasara kubwa na majuto, na kwa miradi ya ujenzi hasara hizo huweza kuwa kubwa sana.

KUCHAGUA UTAALAMU BORA NA SAHIHI UTAKULETEA MATOKEO UTAKAYOJIVUNIA MWISHONI

Sasa ubora namba moja katika ujenzi upo kwenye kutafuta utaalamu sahihi kuanzia kwenye kutengeneza michoro ya ramani na kisha baadaye kwenye kujenga. Kwenye kutengeneza michoro ya ramani ni muhimu sana kujali ubora kwa sababu kuna mambo mengi unaweza usione madhara yake katika michoro ya ramani husika lakini ikaja kukupa changamoto na mateso sana wakati wa kutumia jengo hilo ambapo wakati huo mambo mengi huwezi tena kuyabadilisha na hata amabyo utataka kuyabadili yataambatana na gharama kubwa sana. Hivyo kukosa umakini katika kuchagua mtaalamu sahihi na mwenye uzoefu ni janga kubwa sana unaweza kujiandalia siku za mbeleni hasa katika matumizi ya jengo kwa sababu ukipata mtaalamu sahihi anaweza kukupa hata ushauri sahihi zaidi vile ulivyokuwa unafikiria na kukushawishi ufanye maamuzi bora zaidi kadiri ya taarifa sahihi atakazokuwa anakupa katika mchakato mzima wa kuandaa michoro sahihi ya ramani. Unatakiwa pia kupata mjenzi sahihi na mwaminifu ambaye atazingatia yote anayoelekezwa bila kujali maslahi binafsi na atafanya kazi yenye ubora kwa kuweka ubora mbele zaidi ya faida anayotaka kupata kutoka kwenye ujenzi husika. Ukichangua utaalamu sahihi utakuja kuona manufaa yake mbele na utajivunia uamuzi uliofanya na kinyume chake itakuwa ni hasara na majuto.

KWENYE MIRADI YA UJENZI UTAALAMU SAHIHI NA UZOEFU HAVINA MBADALA

Katika kuchagua utaalamu sahihi unahitajika umakini mkubwa sana kwa upande wako au pengine upate usaidizi kwa watu waaminifu na wenye uzoefu katika mambo ya ujenzi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *