KUFANYA UKARABATI WA JENGO AU KUONGEZA UKUBWA NA KUJENGA HUSISHA MTAALAMU.

Mara kwa mara watu wamekuwa wakifanya ukarabati wa majengo au nyumba zao kwa sababu mbalimbali zikiwemo uchakavu, uharibifu au pale wanapotaka kubadili matumizi au kuboresha jengo lenyewe. Lakini zaidi watu wamekuwa wakiliongeza jengo pia kwa sababu mbalimbali zikiwemo kubadili matumizi, kuongeza matumizi, kukarabati jengo walilonunua kutoka kwenye matumizi ya makazi kwenda kwenye matumizi ya biashara, biashara kukua na hivyo kuhitaji eneo kubwa zaidi ili kuitanua biashara. Lakini pia kutokana na kipato cha mtu kuongezeka na kuona anaweza kumudu nyumba bora na kubwa zaidi watu wamekuwa wakitaka kuongeza nyumba zao ukubwa ili waweze kuishi kwa uhuru zaidi pia ambapo wengi zaidi wamekuwa wakitaka kubadilisha nyumba ya kawaida kwenda kuwa ghorofa.

MABADILIKO KATIKA JENGO LILILOPO YAKIHUSISHA UTAALAMU YANAFANYIKA KWA VIWANGO SAHIHI NA KWA UBORA

Changamoto kubwa ambayo imekuwa ikjitokeza ni watu kutokujua hatua sahihi za kuchukua katika maboresho hayo au katika kuongeza ukubwa ili kupata kitu sahihi na bora wanachohitaji tena kiki katika viwango bora sana ambapo wamekuwa wakitumia mafundi wa kawaida wa kujenga kujadili nao mabadiliko hayo na kuyafanya kienyeji. Hili limesababisha kujikuta aidha wanashindwa kufanya mabadiliko sahihi vile inavyopaswa au kuna baadhi ya mawazo wanakubaliana kwamba hayawezekani au wanaharibu zaidi mtiririko au mpangilio sahihi na kujikuta kazi inakuwa mbaya kuanzia kwenye uzuri, uimara mpaka kwenye matumizi. Hatua sahihi ya kwanza ya kuchukua unapotaka mabadiliko kwanza ni kumwita mtaalamu ambapo kama jengo lina michoro ya ramani iliyotumika zamani katika kulijenga ataanza na hiyo kujadili mabadiliko na kama michoro ya haipo ataitengeneza kutoka kwenye jengo lililopo kwa kuanza kufanya kitu kinachoitwa “documentation”. Mabadiliko yoyote yanawezekana kwa kadiri ya jengo lililopo linavyoweza kuruhusu, ni muhimu sana kutumia mtaalamu kwanza akatengeneza upya michoro ya ramani za mabadiliko katika viwango sahihi na inayozingatia umuhimu wa kila kipengele cha ujenzi husika ili kufikia kile haswa mteja anachotaka bila kuleta sababu yoyote.

UKARABATI AU KUONGEZA JENGO UNAHITAJI KUTUMIA AKILI NA UTAALAMU ZAIDI KULIKO HATA MWANZONI

Kutumia mtaalamu katika kufanya mabadiliko yoyote ya jengo ni muhimu zaidi pengine kuliko hata kwenye kutenegeneza ramani ya jengo jipya kwa sababu ni eneo linalohitaji kutumia akili na utaalamu mkubwa kuliko hata mwanzoni.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *