MAFUNDI WAZURI WA KUJENGA NA “FINISHING” WANAVYOPATIKANA.

Tunaweza kusema fundi ni mzuri wa kujenga kwa kuzingatia mambo mengi, kubwa ikiwa uwezo binafsi unaochangiwa na kujifunza na kufanya kazi nyingi na mbili tunaweza kusema ni uzoefu ambao unatokana na kufanya kazi za aina mbalimbali na kwa namna mbalimbali. Lakini ukiachana na uwezo na uzoefu kuna mambo mengine muhimu kama nidhani binafsi, kuepuka, tamaa, kuweza kujidhibiti dhidi ya vishawishi mbalimbali kama ulevi na madawa ya kulevya ya aina mbalimbali, uwezo wa kujisimamia na kusimamia wengine na uaminifu kuanzia kauli zake mpaka matendo. Huu wote ni mjumuisho wa namna fundi mzuri na bora anavyotakiwa kuwa lakini bado kwa wengine huhitaji pia na usimamizi juu yake wa kuwaongoza ndipo huweza kufikia viwango hivyo vya ubora kwa sababu licha ya ubora wote huo akiachwa kujiongoza mwenyewe bado huwa ni changamoto.

FUNDI MZURI ANAJUMUISHA TABIA NYINGI SANA NA SIO UWEZO WA KIUFUNDI PEKE YAKE

Hivyo sasa mafundi wazuri unaoweza kuwa na uhakika nao kwa 100% ni ambao wako chini ya mwongozo sahihi na ambao wamefanya kazi chini usimamizi mkali na kuongozwa katika mambo mengi katika changamoto nyingi kwa muda mrefu na hivyo tayari wamejenga uwezo wa kufanya kazi kwa namna na utamaduni waliokuwa nao kwa muda mrefu. Uwezo wa kiufundi walioujenga wakiwa chini ya usimamizi huku wakifanya kazi nyingi zenye changamoto mbalimbali, nidhamu ya kazi walioijenga wakiwa chini ya usimamizi sahihi, tabia ya uaminifu iliyojengeka katika mazingira waliyozoea kufanya kazi kwa kujengewa misingi sahihi ya tabia za maeneo ya kazi, adhabu na zawadi walizokuwa wanapewa pale wanafanya makossa na kufanya vizuri kwa kuendana na vigezo tabia na masharti ya maeneo yao ya kazi vyote hivi vimewajenga kujijengea tabia sahihi za kazi na uzoefu unaohitajika katika kuwa fundi bora, sahihi mwenye uwezo na tabia sahihi za zinahitajika katika kufanikisha matokeo yanayohitajika.

MAFUNDI SAHIHI WANAPATIKANA KWA MAPENDEKEZO MAALUM KUTOKA KWA WATU WENYE UZOEFU

Mafundi wa namna hii wanapatikana kwa kupata mapendekezo maalum kutoka kwa watu wenye kuhusika nao, karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *