RANGI YOYOTE YA NYUMBA IKIPAKWA KWA VIWANGO SAHIHI HUPENDEZA.

Watu wamekuwa na machaguo mbalimbali linapkuja suala la rangi za nyumba hasa mpangilio sahihi wa rangi wenye kupendeza na kuvutia. Lakini watu wengi wamekuwa wakitaka kujua mpangilio gani wa rangi unaweza kuwa na maana na mvuto zaidi kupaka katika nyumba zao utakaoongeza mvuto wa nyumba au jengo husika. Kumekuwa na kanuni mbalimbali za mipangilio hii ya rangi katika nyumba na majengo zinazoongozwa na sanaa husika za katika kuleta matokeo fulani yanayotarajiwa yaliyopangwa vizuri katika utaratibu husika. Hata hivyo licha ya kwamba mpangilio sahihi wa rangi huwa unaamua ubora wa matokeo yanayotarajiwa lakini mpangilio pekee hautoshi kuamua ubora wa matokeo yanayotarajiwa baada ya kupaka rangi nyumba au jengo lako.

MBALI NA MPANGILIO SAHIHI WA RANGI, UBORA WA VIWANGO VYA UPIGAJI RANGI PIA UNACHANGIA SANA MUONEKANO BORA

Mpangilio wowote wa rangi, hata kama ni rangi moja ya kawaida ukipakwa katika viwango vya juu vya ubora wa upigaji rangi huwa na matokeo bora na kupendeza sana. Kupaka rangi ni sanaa ambayo inazingatia vitu vingi ili kufikia matokeo bora kuanzia uwezo na viwango mpakaji, uzoefu wa mpakaji n ahata ubora wa bidhaa yenyewe ya rangi pamoja na vifaa na nyenzo anazotumia katika kazi hiyo. Yako majengo mengi ambayo yana muonekano wa kawaida na rangi zake zina muonekano rahisi lakini kutokana na ubora wa viwango vya upakaji matokeo yake yana ubora wa hali ya juu sana yanayojumuisha upevukaji mkubwa wa muonekano wa jengo na vipengele vyake vyote. Mara nyingi hata kama jengo halina mwonekano sahihi wala mvuto kutokana na kazi ya kutengeneza umbo lake ilifanyika katika viwango duni, bado upakaji rangi mzuri unaweza kuliokoa kimuonekano na kulifanya lionekane lina mvuto wa hali ya juu kutokana na umahiri wa upakaji rangi katika viwango vya juu, na hili ni jambo linashauriwa sana kwa majengo ambayo yalikosa ubunifu kwa maumbo yake kutengenezwa kwa viwango duni katika hatua ya kitaalamu ubunifu wa jengo.

UBORA WA VIWANGO VYA UPIGAJI RANGI NYUMBA AU JENGO UNAONGEZA MVUTO WA KIMUONEKANO WA JENGO HATA IKIWA UBUNIFU WAKE ULIKUWA DUNI

Hivyo licha ya kujitahidi katika kuhakikisha unapata mpangilio sahihi wa rangi utakaopendeza na kuvutia ni muhimu zaidi kuhakikisha kwamba unapata wataalam wenye uwezo wa kupaka rangi katika viwango vya juu vya ubora ili kufanikisha hasa kile unacholenga.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *