UJENZI WA HARAKA

Ujenzi wa haraka ni aina ya ujenzi ambao unahitajika kukamilika ndani ya kipindi kifupi sana kwa uhitaji maalumu kwa sababu maalumu. Ujenzi wa aina hii licha ya kwamba unatakiwa kufanyika kwa haraka sana lakini bado unapaswa kuzingatia kanuni zote za ujenzi bora na sahihi na kufuata taratibu za ujenzi kwa sababu jengo husika ni kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu. Uharaka wa ujenzi huu unaweza kuwa ni ujenzi wa nyumba/jengo kukamilika ndani ya kipindi cha kati ya wiki tatu mpaka miezi miwili kutegemea na ukubwa na changamoto za mradi husika.

UJENZI WA HARAKA UNAPASWA KUZINGATIA VIWANGO VYOTE VYA UBORA

Hata hivyo licha ya kwamba ujenzi huu unatakiwa kumalizika ndani ya kipindi kifupi sana bado utahitaji kuanza na michoro ya ramani ambayo kimsingi ndio inayotoa miongozo yote ya ujenzi husika. Hivyo michoro ya ramani kwa ujenzi wa haraka hufanyika na kazi kuanza na huku michoro inaendelea kukamilika na ujenzi nao ukiwa unaendelea. Kwa mfano ramani ya sakafu ya chini ya jengo hufanyika mara moja na kisha jengo kupangilia katika eneo la ujenzi na msingi kuanza kuchimbwa huku michoro mingine ya juu ikiendelea kukamilishwa ambapo mpaka msingi unakamilika unakuta na michoro mingine imemalizika tayari. Hii inatoa nafasi ya kuokoa muda na jengo kukamilika kwa haraka zaidi. Ujenzi wa haraka hufanyika kwa kuweka mafundi wengi katika ujenzi, hatua nyingi za ujenzi kufanyika kwa wakati mmoja na usimamizi makini sana kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa usahihi na kwa muda uliopangwa.

UJENZI WA HARAKA HUJA NA TAREHE MAALUM YA KUWA UMEKAMILIKA NA KILA KITU HUWA KIPO TAYARI KWA AJILI YA KUUKAMILISHA NDANI YA MUDA ULIOPANGWA

Ujenzi wa haraka ni aina ya miradi ambayo hutokea kwa nadra lakini huwa na lengo na uhitaji maalumu ambayo hutakiwa kuwa umekamilika ndani ya kipindi kifupi kwa ajili ya aidha tukio fulani au kama sehemu ya kukamilisha mradi fulani ambao unatakiwa uwe umekamilika kufikia tarehe fulani iliyopo karibu sana. Tuna uzoefu wa miradi kadhaa ya aina hii na imekuwa ni miradi mizuri na inayojenga sana nidhamu ya kazi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *