HATUA TATU MUHIMU KATIKA KUFANYA KAZI YA USANIFU MAJENGO.

Katika kufanya kazi ya kitaalamu ya kufanya na kuandaa michoro ya ramani za usanifu majengo watu wengi wamekuwa wakifikiria mambo kwa ujumla zaidi ndio maana hata wengine wanashindwa kuelewa ukubwa na mchakato wa kazi nzima inavyokwenda. Katika kufanya kazi ya usanifu majengo, kazi nzima imegawanyika katika hatua tatu kubwa ambazo ni hatua ya kazi ya kwanza ni ya kuendeleza wazo na kutengeneza michoro ya mwanzoni(preliminary design stage), hatua ya kazi ya pili ni kazi ya kuboresha kazi wazo na kuboresha michoro iwe katika viwango sahihi na katika uhalisia zaidi wa kuweza kujengwa pamoja na kuandaa picha za muonekano wa jengo katika pande zote na kutoka katika pembe zote, hatua ya kazi ya ni kutengeneza michoro ya mwisho ya kwa ajili ya ujenzi ambayo itajumuisha aina zote sita za michoro pamoja na kuhakikisha taarifa zote muhimu katika michoro zimejumuishwa na mahesabu yote ya namna kazi inakwenda kufanyika imejumuishwa pia.

MAJADILIANO YA KAZI YA USANIFU MAJENGO NDIO MSINGI WA KAZI BORA ILIYOTOKANA NA KUELEWANA KWA USAHIHI

Kutokana na kazi kugawanyika katika hatua tatu kubwa gharama ya jumla nayo imegawanyika mara tatu katika theluthi tatu. Katika hatua ya kwanza theluthi moja ya kiasi cha fedha yote kinalipwa na kazi inafanyika mpaka kukamilisha hatua hiyo ya kwanza ambapo wazo husika linafanyiwa kazi kwa kiasi kilichoeleweka kisha baada ya hapo kazi husika inajadiliwa kuhakikisha kwamba muafaka unafikiwa na pande zote zinaridhika kwa kiasi ambacho kimeafikiwa. Baada ya hapo inafuata hatua ya pili ambapo mawazo ya mwanzo yanaboreshwa na kuifikisha kazi katika hatua ya ukamilifu na hitimisho pamoja na kufanyia kazi mwonekano wa nje wa jengo unaojumuisha vipengele vyote vya ujenzi ambavyo havipo katika ramani ya chini bali mwonekano wa wima. Baada ya hatua hii ya hitimisho na mwonekano wa nje kitalipwa kiasi kingine cha fedha cha theluthi moja ya kiasi chote kilichokubaliwa kisha kama kuna mabadiliko tena yatafanyiwa kazi kabla ya kuingia hatua ya mwisho. Baada ya hapo kazi itaingia kwenye hatua ya mwisho ambayo ni kutengeneza michoro ya mwisho katika seti saba muhimu au zaidi na kisha kuprinti katika nakala ngumu zisizopungua tatu na kupiga mihuri michoro hiyo kama kuna uhitaji huo kisha kukabidhi michoro ya ramani husika na kisha kumalizia theluthi ya mwisho ya malipo iliyobakia.

HATUA ZA KAZI NA MAJADILIANO HUPELEKEA MATARAJIO MENGI YA MTEJA KUFIKIWA KATIKA NAMNA AMBAYO INAKUBALIKA KITAALAMU

Mchakato huu umekaa kwa uwazi na kwa namna ambayo inatoa uhuru wa kufikia viwango bora sana vya kazi huku malipo yalifanyika kwa namna ambayo inaleta msukumo wa kazi kufanyika kwa ubora na kumalizika kwa muda na kwa usahihi ulioridhiwa na pande zote.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *