KILA MAAMUZI UNAYOFANYA KATIKA UJENZI YANA FAIDA KUBWA MBELENI NA KINYUME CHAKE NI HASARA NA MAJUTO.

Nimekuwa nikisisitiza sana suala la kuzingatia ubora wa huduma katika kila hatua ya ujenzi. Hii ni kwa sababu nafahamu kwamba hakuna mtu aliyewahi kujutia huduma bora bila kujali alizipata kwa namna gani, kwa sababu huduma bora siku zote zitakupa furaha na ufahari baadaye. Hisia zinazotuingia na kututia hofu tukaogopa huduma bora kwa kuhofia kwa gharama ni hisia zinazotupoteza kwa sababu mwisho wa siku hiyo ni hofu tu, ambayo inakuwa na nguvu kabla hujalipa hiyo gharama lakini ukishalipa gharama husika huwa unasahau na kubaki kungoja furaha na ufahari mbele ikiwa umefanya maamuzi sahihi, lakini ukiongozwa na hofu ya kuhofia sana gharama na ikapelekea ukafanya maamuzi yasiyo sahihi ya kushindwa kuchagua ubora wa huduma basi utakuwa unasubiri hasara, maumivu na majuto. Jambo la muhimu sana la kuzingatia katika eneo hili ni kutumia fikra na akili katika kutazama upande wa faida na hasara kabla ya kufanya maamuzi husika ambayo hayatakiwi kuongozwa na hisia za hofu bali mantiki ili uweze kuchagua iliyo sahihi badala ya kuangalia urahisi peke yake bila kuzingatia usahihi.

FURAHA NA UFAHARI VITALETWA NA MAAMUZI SAHIHI UTAKAYOFANYA MWANZONI

Kwa mfano tunajaribu kusisitiza kwamba kabla mtu hajaanza kufanya kazi ya ujenzi kutafuta utaalamu sahihi ambapo atatengeneza michoro sahihi ya ramani ya ujenzi itakayotoa mwongozo bora sahihi kabisa katika kujenga huku kila kitu kikiwa wazi na kinaeleweka kwa usahihi kuanzia mwanzoni mpaka kinapokamilika. Miradi ya ujenzi ni miradi inayohusisha gharama kubwa sana kuanzia kuanza mpaka kukamilisha, hivyo itakuwa ni maamuzi yasiyo sahihi kabisa mtu kwa kubaki na hofu ya kuogopa gharama anafanya maamuzi yasiyo sahihi ya kujiingiza kwenye kufanya kazi itakayomgharimu mamilioni ya pesa lakini isiyo ya viwango bora. Viwango bora vya ujenzi vinaaniza kwenye mpangilio sahihi wa jengo lenyewe ambalo limezingatia mambo yote muhimu na haswa mapendekezo na mahitaji ya mteja mwenyewe, pia kila kitu kiwe kimeeleweka tangu mwanzoni ili katika utekelezaji ijulikane wazi nini haswa kinachotarajiwa kama matokeo ya mwisho. Hivyo ikiwa maamuzi ya mwanzoni yamefanyika kwa usahihi na maamuzi ya kuchagua usimamizi sahihi nayo yamefanyika kwa usahihi pamoja na ufuatiliaji wa karibu unaozingatia kanuni sahihi za kila kinachoenda kufanyika basi mwishoni ni furaha na ufahari wa kuweza kufanya maamuzi hayo muhimu.

MATOKEO YA MAAMUZI UNAYOFANYA YANAKUJA MWISHONI NA HIYO NDIO CHANGAMOTO KUBWA ZAIDI

Changamoto ya kufanya maamuzi kwa kutumia hisia kwa hofu ambazo ni hisia tu yakapelekea uharibifu huwa haionekani mwanzoni wakati wa kufanya maamuzi, hii huja mwishoni baada ya uharibifu kuwa umefanyika hivyo ni vyema kujitahidi sana kuwa makini na hili kwani shida yake haitaonekana wakati sahihi, kwa hiyo inapaswa mtu kuwa mjanja na kujiongeza mapema katika hili.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *