TOVUTI YETU YA UJENZI MAKINI NI KWA AJILI YA KUJIFUNZA KWA MAELEZO NA PICHA.

Katika tovuti yetu ya ujenzi makini tumekuwa tukiandika makala nyingi za aina mbalimbali kuanzia makala za kitaalamu, kiufundi, miongozo, maelekezo, ushauri n.k. Lakini pia tumekuwa tukiambatanisha na uhalisia katika picha ya vitu mbalimbali japo sio picha zote huendana na ujumbe moja kwa moja lakini angalau picha hizi huweza kujenga hamasa na kumjengea msomaji picha ya kimazingira ya kile anachosoma katika kumsaidia kuvuta mazingira halisi wakati akiendelea kusoma. Kwa sababu tumelenga zaidi kuongeza uelewa kwa ujumla kwa watu katika kila kitu kuanzia mambo ya ufundi mpaka machaguo mbalimbali ambayo mara nyingi mteja hufanya hivyo tunaandika kila kitu kwa namna mchanganyiko.

TUNAJARIBU KUONGEZA UELEWA WA MAMBO MUHIMU KUHUSU UJENZI ILI KUPUNGUZA CHANGAMOTO NA HASARA AMBAZO HUJITOKEZA MARA KWA MARA

Lengo hasa la kuandika makala hizi mfululizo ni kuongeza uelewa wa mambo ya ujenzi kwa ujumla sambamba na kujaribu kujibu maswali mengi ambayo huwatatiza watu wengi na wakati mwingine kuwasababishia matatizo na hasara za namna mbalimbali. Hata hivyo ikiwa watu wanahitaji ushauri zaidi wa chochote ambacho aidha hawajakielewa kwa usahihi au hawajapata maelezo yanayojitosheleza katika makala husika basi ndio maana tunaweka mawasiliano ya simu ili mtu awe huru kupiga na kuuliza katika kupata ufafanuzi zaidi wa kile anachohitaji kukifahamu kwa undani zaidi. Katika tovuti hii tunaweka picha za kazi mbalimbali za kisanifu na za ujenzi ambazo zimefanyika katika kuonyesha mambo yanavyofanyika katika uhalisia ili kwanza kujenga imani na watu wanaoitembelea tovuti hii kwamba ushauri tunaotoa ni wa uhakika kwa sababu sisi wenyewe tunajihusisha na kazi hizi kila siku hivyo tunafahamu kwa undani kile tunachozungumza, na pili ni kumwezesha mtu kuitumia kama mifanp hai sehemu ya kuanzia ikiwa ana maswali zaidi baada ya kuona mifano hai ya kinachofanyika.

TUNAHITAJI KUSIKIA MAWAZO MBADALA PAMOJA NA CHANGAMOTO KUTOKA KWA WATU MBALIMBALI ILI TUWEZE KUBORESHA ZAIDI HUDUMA ZETU, KUONGEZA THAMANI

Hivyo tunahimiza kwamba ikiwa mtu ana maswali, maoni, ushauri, nyongeza au mawazo mengine yoyote mbadala anakaribishwa tuwasiliane na kusaidiana katika kuendelea kutoa huduma bora zaidi zitakazosaidia kuongeza thamani zaidi katika miradi ya ujenzi ya aina zote.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *