NYASI NA MITI/MSITU KWENYE BUSTANI YA NYUMBANI HUONGEZA THAMANI YA ENEO.

Mpangilio wa bustani katika eneo la makazi bado limeendelea kuwa ni suala lisilopewa kipaumbele na watu wengi kwa sababu ya kutokuwa na utamaduni wa kujali sana kuhusu bustani.

Lakini kwa mtu yeyote anapotembelea katika eneo ambalo limepangilio kwa usahihi kwenye masuala ya bustani huwa anaona wazi ni jinsi gani eneo hilo limeongezeka thamani kwa sababu ya uwepo wa bustani nzuri za miti, maua na nyasi zilizopangiliwa vizuri.

MCHANGANYIKO WA NYASI, MITI, MAUA NA MISITU YA MITI INAONGEZA SANA HADHI YA ENEO

Kama nilivyoshirikisha katika makala zilizopita kwamba eneo linalokuwa na sakafu ngumu kama ya zege, lami au vigae vya ardhini(paving) linatakiwa kupungua kadiri inavyowezekana na nafasi yake kuchukuliwa na bustani za miti, nyasi, maua na misitu midogo ya miti.

Ikiwa eneo kutokana na kutokana na kutokuwa kubwa vya kutosha linalazimu eneo kubwa kuwekwa ardhi ngumu kama sakafu ya lami, zege au vigae vya ardhini basi miti na misitu ya miti inatakiwa kupewa kipaumbele zaidi ili kuongeza mzunguko mkubwa wa hewa utakaosaidia eneo hili kuwa na ile thamani ya mazingira asili.

ARDHI LAINI(SOFT LANDSCAPE) INAPASWA KUTAWALA ISIPOKUWA KWA MAENEO YENYE ULAZIMA WA KUWEKA SAKAFU NGUMU(HARD LANDSCAPE) KWA SABABU YA UHITAJI

Lakini hata ikiwa kama eneo ni kubwa kiasi kwamba maeneo yanayowekwa nyasi ni makubwa, bado eneo litavutia zaidi na kuongezeka thamani zaidi ikiwa kutakuwa na miti mingi pamoja na misitu ya miti na maua ambayo itaboresha sana mzunguko wa hewa katika mazingira ya nyumbani kwa ujumla.

Hivyo suala la bustani ya nyumbani mbali na kujali kuhusu maeneo ya maegeso ya magari pamoja na maeneo mengine yanayohitaji kuwekwa sakafu ngumu lakini kupaumbele kinapokuwa katika ardhi laini yenye nyasi kwa wingi, bustani za miti na misitu ya miti pamoja na maua eneo linaongezeka sana thamani na kuongeza sana thamani ya maisha ya wakaazi wa eneo hilo.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *