UJENZI WA MAJENGO NA ATHARI ZA KIMAZINGIRA (ENVIRONMENTAL IMPACT ASSESSMENT(EIA)”.

Miradi mingi ya ujenzi hasa miradi mikubwa huwa na athari kubwa zaidi za kimazingira katika mazingira ambayo mradi unakuwepo ambayo huleta madhara kwa wakaazi wa eneo husika. Hivyo kuna vigezo vya athari za kimazingira vilivyowekwa na mamlaka zinahusika ili kuruhusu mradi kufanyika.

Athari za kimazingira za mradi ziko za aina nyingi sana kama jinsi ilivyo kwa aina za uharibifu wa kimazingira zilivyo nyingi kuanzia sauti, hewa, maji, ardhi n.k., kadiri ya aina na asili ya mradi wenyewe sambamba na asili ya aina, watu au shughuli za kijamii zilizopo katika eneo husika.

MRADI WA UJENZI WA ENEO LA VIWANDA NA ATHARI ZA KIMAZINGIRA

Mtu unapofikiria kufanya mradi wa ujenzi hasa mradi mkubwa ni muhimu sana kutafuta mtaalamu wa mazingira wa kufanya na kukuandikia ripori ya uchunguzi wa kimazingira wa eneo hilo(Environmental Impact Assessment) ili kujiridhisha kama mradi husika unafaa kujengwa maeneo hayo.

Ripoti hii ya kimazingira itapelekwa katika kitengo cha mazingira katika halmashauri husika ambayo kupitia ripoti hiyo ndipo mamlaka husika zitaamua kama kuruhusu au kutoruhusu mradi huo kadiri ya jinsi ulivyo na madhara kwa watu wa eneo husika.

UKUBWA WA ATHARI ZA KIMAZINGIRA UNATOKANA NA AINA NA ASILI YA MRADI HUSIKA WA UJENZI

Hata hivyo kuna miradi ambayo inajulikana wazi kwamba athari zake za kimazingira ni kubwa zaidi kuliko miradi ya aina nyingine, kwa mfano miradi ya viwanda vizito(heavy industries), migodi ya machimbo ya madini, kumbi za starehe na mikutano, n.k., ni aina ya miradi yenye athari kubwa zaidi za kimazingira ukilinganisha na miradi kama ya nyumba za makazi ya watu pekee.

Ni muhimu na salama zaidi kuhusisha wataalamu wa mazingira hata kwa ushauri tu wa mwanzoni peke yake upate mtazamo wao juu ya mradi husika katika eneo hilo kabla hujaingiza pesa nyingi.

Architect Sebastia Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *