KIWANJA KINACHOFAA KUJENGA SHULE AU MAJENGO YA TAASISI NYINGINE YOYOTE.

Kwenye sekta ya ujenzi, moja kati ya changamoto kubwa ambayo watu huwa wanakutana nayo mara kwa mara ni ujenzi kukwama kwa sababu ya vigezo na masharti vilivyowekwa na mamlaka husika. Japo wakati mwingine sheria inaacha nafasi ya kuwepo kwa mabadiliko lakini bado changamoto ni kubwa.

Suala la ujenzi kukwama kwa sababu ya kuwepo kwa masharti na vigezo vingi linatokana na watu kutokuwa wafuatiliaji wa karibu wa sheria zilizowekwa na mamlaka husika za kiserikali kabla ya kuanza mchakato wa utekelezaji wa mradi wake.

Kila taasisi inayotaka kujengwa kuna wizara ya serikali ambayo inahusiana na taasisi husika ambapo wizara hiyo imeweka vigezo na masharti yanayotakiwa kutimizwa kuhusiana na mradi huo ili mradi husika uruhusiwe kuendelea kujengwa.

KUJENGA SHULE AU TAASISI NYINGINE YA KIJAMII KUNA VIGEZO NA MASHARTI YA MAMLAKA HUSIKA UNAPASWA KUTIMIZA ILI KUEPUKA USUMBUFU NA HASARA

Kwa mfano taasisi kama shule ya msingi, sekondari, chuo cha ufundi, chuo kikuu, n.k., kuna masharti ambayo wizara ya elimu imeweka kuhusiana na majengo husika kuanzia ukubwa wa kiwanja unaohitajika, ukubwa wa vyumba vya madarasa, majengo na matumizi mengine yanayohitajika kuwepo n.k.

Hilo lipo hata kwa taasisi nyingine kama hospitali, vituo vya afya, maabara, zahanati, viwanda, masoko, maktaba za kijamii, viwanja vya mpira n.k., kila kimoja na wizara husika.

NI VYEMA KABLA HUJAANZA KUJENGA TAASISI YOYOTE KUANZA KWANZA KUFUATILIA VIGEZO NA MASHARTI VILIVYOWEKWA KUHUSIANA NA MAJENGO HUSIKA

Hivyo pale mtu unapoanza kufikiria kuhusu kujenga shule au taasisi yoyote ya kijamii mara baada ya kufanya maamuzi kwamba unakwenda kujenga taasisi hiyo jambo la kwanza kabisa unalopaswa kuanza nalo ni kufika katika wizara husika na kupewa vigezo na masharti kisha kuanza mchakato wa utekelezaji huku ukizingatia vigezo na masharti husika.

Kwa kuanza hivi utapunguza sana usumbufu katika utekelezaji wa mradi wako na kuepuka kufanya makosa ambayo yanaweza kukupelekea kukwama au kupata hasara ambayo hukuitarajia mwanzoni.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *